Pata taarifa kuu
KOREA KUSINI

Rais mpya wa Korea Kusini Moon Jae-in aanza kazi baada ya kuapishwa

Rais wa mpya wa Korea Kusini Moon Jae-in ameapishwa leo baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi wa urais uliofanyika siku ya Jumatatu.

Rais mpya wa Korea Kusini Moon jae-in
Rais mpya wa Korea Kusini Moon jae-in 路透社
Matangazo ya kibiashara

Moon anaanza kazi  akiwa na wakati mgumu wa kupambana na ufisadi lakini pia kushughulikia suala tata la usalama hasa kutokana na vitisho vya Korea Kaskazini.

Wakati uo huo, anakabiliwa na changamoto ya kidiplomasia kati ya nchi yake na Marekani ambayo imeweka mitambo yake ya kuzuia mashambulizi kutoka Korea Kaskazini.

Aidha, rais huyu mpya hata kabla ya kuchaguliwa, amekuwa akisema ana nia ya kuzungumza na Korea Kaskazini na kubadilisha sera ya Seoul.

“Nitaenda  Beijing na Tokyo na hata Pyongyang katika mazingira mazuri,” alisema Moon baada ya kuapishwa.

“Ikiwa nitahitajika, nitakwenda Washington mara moja,” aliongeza.

Rais huyo mpya amesema atakuwa kiongozi wa raia wote wa Korea Kusini.

Tayari amemtaja mwanahabari wa zamani wa zamani Lee Nak-Yon, kuwa Waziri Mkuu wake.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.