Pata taarifa kuu
KOREA KUSINI-UCHAGUZI SIASA

Korea Kusini yampata rais mpya

Moon Jae-in amechaguliwa na raia wa Korea Kusini kuwa rais mpya nchi hiyo.Moon Jae-in anatarajiwa kuapishwa siku ya Jumatatu. Anatarajiwa kuchukua nafasi ya rais wa zamani Park Geun-hye aliyetimuliwa mdarakani kwa tuhuma za ufisadi.

Moon Jae-in asherehekea ushindi wake katika uchaguzi wa urais nchini Korea Kusini, Jumanne, Mei 9, 2017.
Moon Jae-in asherehekea ushindi wake katika uchaguzi wa urais nchini Korea Kusini, Jumanne, Mei 9, 2017. REUTERS/Kim Hong-Ji
Matangazo ya kibiashara

Ripoti kutoka nchini Korea Kusini zinasema kuwa, Moon kutoka chaka cha Kiliberali, amepata ushindi wa asilimia 41.4 huku mpinzani wake wa karibu Hong Joon-Pyo akipata asiimia 23.3.

Kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 20, asilimia 77.2 ya wapiga kura walijitokeza kushiriki katika uchaguzi huu.

Mamilioni ya wafuasi wa Moon wamekusanyika jijini Seol kusherekea ushindi huu.

Wakati wa kampeni za urais Moon aliahidi kujaribu kufanya mazungumzo na jirani yake Korea Kaskazini na kubadilisha kubadilisha sera ya nchi yake kutozungumza na Pyonyang.

Mwanajeshi huyo wa zamani na wakili wa maswala ya haki za binadamu anatarajiwa kuapishwa siku ya Jumatatu.

Anatarajiwa kuchukua nafasi ya rais wa zamani Park Geun-hye aliyeondolewa mdarakani mwezi Machi kwa tuhma za ufisadi ambazo ameendelea kusema zimechochewa kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.