Pata taarifa kuu
BURMA-USALAMA

Mapigano makali yatokea nchini Burma karibu na China

Machafuko mapya yametokea nchini Burma. Watu wasiopungu thelathini waliuawa Jumatatu hii Machi 6 katika jimbo la Shan , kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo karibu na mpaka na China: waasi 20, askari watano na raia watano wameuawa.

Waasi wa kundi la MNDAA katika kambi ya kijeshi katika mji wa Kokang, Machi 11, 2015.
Waasi wa kundi la MNDAA katika kambi ya kijeshi katika mji wa Kokang, Machi 11, 2015. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo imetolewa na serikali ya Burma, huku ikisema kuwa waasi waliendesha shambulizi hilo la kusha ngaz mapema asubuhi katika mapema asubuhi.

Waasi wa kundi la MNDAA (Myanmar National Democratic Alliance Army), ambapo baadhi yao waliokuwa wamevaa sare ya polisi, kwanza walishambulia vituo vya jeshi na polisi, kwa mujibu wa ofisi ya Aung San Suu Kyi. Kisha kundi jingine lilishambuliwa maeneo kadhaa katika mji wa Shan.

Video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zimeonyesha kile kinachoonekana kuwa sehemu ya mji ikiwaka moto, huku wakaazi wa baadhi ya maeneo wakikimbilia katika maeneo yenye usalama. Milipiko ya mabomu na milio ya risasi vimesikika siku nzima,

Muungano wa kaskazini, ikiwa ni pamoja na kundi la waasi la MNDAA, umeandika kwenye Facebook, kwamba wanajihami dhidi ya operesheni za askari wa Burma wanazoendesha tangu mwezi Desemba katika mji wa Kokang. Katika jimbo hilo mapigano makali yanashuhudiwa tangu mapema mwaka 2015, wakati ambapo maelfu ya watu walilazimika kukimbia mapigano wakielekea China.

Baada ya kushinda uchaguzi 2015, Aung San Suu Kyi aliweka kipaumbele katika mchakato wa amani na kabila za watu wachache wenye silaha. Lakini tangu kuingia madarakani, mapigano kati ya waasi na jeshi yameongezeka kwa kiasi kikubwa. Kulingana na katiba iliyoandaliwa na jeshi, Aung San Suu Kyi hana mamlaka yoyote kwa jeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.