Pata taarifa kuu
UTURUKI-USALAMA

Shambulizi baya latokea katika mji wa Izmir

Nchini Uturuki, siku tano baada ya shambulizi dhidi ya klabu ya burudani mjini Istanbul na kuuawa watu 39, shambulio jingine lilitokea Alhamisi hii mchana katika mji wa Izmir. Bomu lililotegwa katika gari lililipuka mbele ya jengo la mahakama mjini Izmir.

Polisi ya Uturuki yachunguza dalili katika eneo la shambulio.
Polisi ya Uturuki yachunguza dalili katika eneo la shambulio. REUTERS/Tuncay Dersinlioglu
Matangazo ya kibiashara

Watu wawili wameuawa akiwemo polisi mmoja na watu sita kwaliojeruhiwa. Wawili kati ya washambuliaji waliuawa, mshambuliaji watatu bado anatafutwa. Pamoja na muhusika mkuu katika shambulizi la mjini Istanbul ni magaidi wawili ambao wanasakwa kwa sasa nchini Uturuki .

Washambuliaji walikua na lengo la kuendelea na mashambulizi mbalimbali, na hali hiyo ingelisababisha maafa makubwa. washambuliaji hao watatu waliokua katika gari hilo lililokua limejaa vilipuzi waliondoka katika gari hilo kabla hawajalilipua. Lakini nia yao ilikua kuendesha mbashambulizi mbalimbali katika mji huo.

bunduki za kivita zimepatikana karibu na miili ya magaidi wawili waliouawa na si chini ya guruneti nane zilizopatikana. wakati huo huo kuna gari jingine dogo lililokua limejaa vilipuzi ambalo lilipatikana kando na gari hilo lililolipuliwa. Hata hivyo polisi iliingilia kati na kuweza kulidhibiti gari hilo kabla halijalipuka.

Mlipuko huo ulitokea mbele ya kituo cha magari karibu na mahakama ya mjini Izmir.

Siku tano baada ya shambulizi dhidi ya klabu ya burudani mjini Istanbul, kuna uwezekano kuwa shambulizi hili liliendeshwa na kundi la Islamic State, lakini Mkuu wa mkoa wa Izmir tayari amesema kuwa shambulizi huenda liliendeshwa na kundi la waasi la PKK.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.