Pata taarifa kuu
CHINA-AJALI

Watu zaidi ya 67 wapoteza maisha nchini China baada ya jengo kuporomoka

Watu wasiopungua 67 wamepoteza maisha Alhamisi hii nchini China baada ya jengo moj lililokua likijengwa kuporomoka katika kituo cha umeme katika mkoa wa Jiangxi, mashariki mwa China

Eneo la ajali Alhamisi, Novemba 24, 2016 katika mji wa Fengcheng, Jiangxi.
Eneo la ajali Alhamisi, Novemba 24, 2016 katika mji wa Fengcheng, Jiangxi. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Waanyakazi kadhaa bado wamenaswa chini ya vifusi, televisheni ya serikali imearifu. Katika ajali hiyo watu watano waliojeruhiwa wamepelekwa hospitalini.

Ajali hiyo ilitokea saa 1:00 asubuhi saa za China (sawa na saa 5:00 usiku saa za kimataifa) katika eneo la Fengcheng, kwenye mnara ambao bado unajengwa. Waziri Mkuu Li Keqiang, ameagiza uchunguzi haraka.

Ajali mbaya katika maeneo ya viwanda huwa zikitokea mara kwa mara nchini China. Mwaka jana, mlipuko mkali wa kemikali ulitokea katika mji wa Tianjin, katika pwani ya kaskazini mwa nchi hiyo, na kuua zaidi ya watu 170.

Rais Xi Jingping ameahidi kwamba serikali itajifunza kupitia matukio mabaya yaliyotokea katika migodi, viwanda au mitambo ya umeme katika miongo mitatu ya ukuaji mkubwa wa kiuchumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.