Pata taarifa kuu
UFILIPINO-USALAMA

Rais wa Ufilipino atuhumiwa mauaji

Mtu aliyejitambulisha kama "muuaji" aliyetubia kwa Mwenyezi Mungu anamtuhumu Rais wa Ufilipino Rodrigo Dulerte kuwa alimuua afisa wa serikali na kuamuru mauaji ya wapinzani alipokuwa Meya.

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte Septemba 5, 2016.
Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte Septemba 5, 2016. REUTERS/Lean Daval Jr
Matangazo ya kibiashara

Shutma dhidi ya Rodrigo Duterte imetolewa mnbele ya baraza la Seneti la Ufilipino na Matobato Edgar, ambaye ana umri wa miaka 57.

Alikuwa akihutubia kamati ya Baraza la Seneti inayohusika na kuchunguza kuhusu kuongezeka kwa mauaji tangu kuwasili kwa rais Rodrigo Dulerte madarakani mwezi Juni.

"Watu walioandaliwa kufanya mauaji hayo" ni pamoja na askari polisi na waasi wa zamani wa kikomunisti kwa amri ya Rodrigo Duterte ambao waliua maelfu ya watu katika kipindi cha miaka 25, kwa mujibu wa Edgar Matobato.

"Madai ya mwendawazimu"

Edgar Matobato amesema baadhi ya wahanga walinyongwa, wengine walichomwa moto au kukatwa vipande vipande.

Mtoto wa rais wa Ufilipino, Paolo Duterte, amefutilia mbali shutma hizo, akimuita Edgar Matobato kuwa ni "mwendawazimu".

"Sintosita kujibu katika mashtaka kuwa bwana huyo ni mwendawazimu," Paolo Dulerte amesema.

Rodrigo Duterte alikabiliwa nashutuma mbalimbali za ukiukwaji wa haki za binadamu.

Alichaguliwa juu ya ahadi ya kuyaangamiza makundi ya wafanyabisahara ya madawa ya kulevya nchini Ufilipino.

"Vita dhidi ya madawa ya kulevya" vililvyofanywa na serikali yake vilisababisha mamia ya watu kuuawa katika miezi michache.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.