Pata taarifa kuu

Watu 3 wauawa katika shambulizi la bomu mashariki mwaUturuki

Kwa uchache watu watatu wameuawa na wengine 120 kujeruhiwa Alhamisi hii katika shambulio la bomu lililotegwa katika gari, shambulio ambalo lilitokea katika mji wa Elazig, mashariki mwa Uturuki. Mji huu ulikua bado haujaguswa na mapigano kati ya vikosi vya serikali na waasi wa Kikurdi, chanzo cha usalama kimebaini.

Askari wa Uturuki wakifanya mazoezi katika mji wa  Cizre,kilomita 10 na mpaka kati ya Uturuki na Iraq  Juni 5, 2007.
Askari wa Uturuki wakifanya mazoezi katika mji wa Cizre,kilomita 10 na mpaka kati ya Uturuki na Iraq Juni 5, 2007. (Photo : AFP)
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hili, lililohusishwa waasi wa Kikurdi, limetokea saa moja baada ya shambulio jingine la bomu lililotegwa katika gari ndogo ambalo limewaua watu watatu katika mji wa Van, pia mashariki mwa Ukraine.

Shambulio la Elazig limelenga makao makuu ya polisi ya mkoa huu na kusababisha uharibifu mkubwa katika jengo la ghorofa nne - ambalo lina makazi ya familia za askari polisi, na majengo jirani, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Uturuki.

Idadi kubwa ya watu waliojeruhiwa inaonyesha kuwa ukubwa wa mlipuko huo, na huenda idadi ya vifo ikaongezeka.

Elazig ni mkoa wa mashariki, wenye wakazi ambao si Wakurdi ulikua mpaka sasa haujaguswa na mapigano kati ya vikosi vya Uturuki na waasi wa Kikurdi wa kundi la PKK, ambalo limekua likiendesha mashambulizi ya mara kwa mara kusini mashariki mwa nchi.

Serikali imeahidi kuendeleza oparesheni zake kwa lengo la kulivunja kundi la waasi la PKK mashariki mwa Uturuki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.