Pata taarifa kuu
THAILAND-USALAMA

Mfululizo wa mabomu yalenga maeneo ya kitalii kusini mwa Thailand

Maeneo matatu, eneo la mapumziko la Hua Hin, Phuket na Surat Thani, kusini mwa Thailand, yamekubwa na mfululizo mashambulizi ya mabomu usiku wa Alhamisi hadi Ijumaa hii asubuhi.

Askari polisi wa Thailand apiga doria anasimama katika eneo la la mashambulizi mjini Hua Hin, Agosti 12 baada ya milipuko miwili.
Askari polisi wa Thailand apiga doria anasimama katika eneo la la mashambulizi mjini Hua Hin, Agosti 12 baada ya milipuko miwili. MUNIR UZ ZAMAN / APF / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya mwisho inasema mashambulizi hayo yamesababisha vifo vya watu wanne na wengine wengi kujeruhiwa.

Milipuko hiyo inatokea siku moja kabla na siku ya kuzaliwa ya Malkia Sirikit, tarehe muhimu katika kalenda ya Thailand, lakini sababu ya mfululizo huu wa mashambulizi bado haijajulikana.

Mabomu mawili ya kwanza yalilipuka yakifuatana baada ya dakika ishirini baa iliyo katika eneo la mapumziko la Hua Hin kusini mwa mji wa Bangkok. Saa chache baadaye, mlipuko wa tatu ulisikika katika mji wa Surat Thani, kilomita 400 kusini mwa mji wa Hua Hin.

Hata hivyo, mji huu wa Hua Hin umelengwa na mashambulizi kwa mara ya pili Ijumaa hii asubuhi pamoja na katika eneo la mapumziko la Phuket, kusini mwa nchi hiyo, ambapo milipuko miwili imesikika na kusababisha mtu mmoja kujeruhiwa.

Mji wa Hua Sin, uliyokumbwa na mashambulizi hayo, ni maarufu sana kwa watalii wa ndani na wale kutoka nchi za kigeni hasa wakati ambapo mwisho wa juma umeanza kutokana na maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa Malkia wa Thailand Ijumaa hii.

sababu za mashambulizi bado hazijulikani

Polisi bado haijaju sababu za mashambulizi. Baadhi ya wachambuzi wanabaini kwamba mashambulizi hayo yanatokea siku chache tu kabla ya maadhimisho ya kwanza ya mashambulizi yaliyosababisha vifo vya watu wengi Agosti 17 mwaka jana, karibu na hekalu ya dini la Hindu mjini Bangkok.

Shambulizi hili lilitekelezwa na kabila la Uighurs kutoka China, ambao hawakuridhishwa kufukuzwa kwa baadhi ya ndugu zao na serikali ya Bangkok kwenda China.

Wengine wanadhani kuwa mashambulizi haya yanahusiana na mvutano wa kisiasa wa ndani wakati ambapo katiba iliyoandikwa chini ya usimamizi wa utawala wa kijeshi uliyo madarakani imepitishwa kwa kura ya maoni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.