Pata taarifa kuu
JAPAN-AKIHITO

Mfalme wa Japan Akihito aomba kuachia ngazi

Mfalme Akihito, mwenye umri wa miaka 82, ameonyesha Jumatatu hii wasiwasi wake kuhusu uwezo wake wa kuendelea kutimiza wajibu wake, na kupendekeza kuwa anaendelea kusubiri mabadiliko katika sheria ambazo zinamuamuru kubaki Mfalme mpaka pale utafikia mwisho wa maisha yake.

Mfalme wa Japan, Akihito,wakati akishrehekea miaka 82 ya kuzaliwa kwake,  Tokyo, Desemba 23, 2015.
Mfalme wa Japan, Akihito,wakati akishrehekea miaka 82 ya kuzaliwa kwake, Tokyo, Desemba 23, 2015. REUTERS/Thomas Peter/File
Matangazo ya kibiashara

Mpaka sasa, hakuna Ibara yoyote kisheria inayomruhusu Mfalme kuondoka mamlakani nchini Japan.

"Kwa bahati nzuri, afya leo inaendelea vizuri. Hata hivyo, ninapoona afya yangu inapodhoofika hatua kwa hatua, ninakua na wasiwasi wa kutimiza majukumu yangu kama ishara ya serikali," amesema katika hotuba iliyorushwa kwenye runinga, akitoa mfano wa umri wake na haja ya kutoweza kikamilifu majukumu yake.

Mfalme Akihito, akielezea mawazo yake, amesema kuwa hawezi "kutoa maelezo maalum juu ya mfumo wa kifalme."

Hata hivyo Mfalme Akihito ameeleza nia yake ya kutaka kuachia ngazi katika uongozi wa taifa la Japan.

Muda mfupi baada ya hotuba yake, Waziri Mkuu, Shinzo Abe, amesema atatathmini uangalifu mkubwa madai ya mfalme huyo.

Mfalme Akihito amekuwa madarakani tangu kifo cha babake, Hirohito, mwaka 1989, na anaongoza nchi hiyo kwa muda wa mika 27 sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.