Pata taarifa kuu
INDIA-AJALI-USALAMA

India: watu zaidi ya 100 wapoteza maisha katika ajali ya moto

Watu zaidi ya 100 walipoteza maisha katika usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili kufuatia ajali ya moto iliyotokea katika hekalu, kusini magharibi mwa India, wakati watu walipokusanyika kuangalia fataki zinavyorushwa.

Wanawake wakifanya maombi Februari  26, 2013 katika jimbo la Kerala.
Wanawake wakifanya maombi Februari 26, 2013 katika jimbo la Kerala. AFP
Matangazo ya kibiashara

Watu wengine zaidi ya 250 wamejeruhiwa katika tukio hilo ambalo linakisiwa kuwa limesababishwa na mlipuko ambao haukudhibitiwa wa kifaa katika hekalu yaDevi Puttungal ya watu kutoka jamii ya Wahindu katika mji wa pwani wa Paravur, katika jimbo la Kerala, wakati wa maadhimisho yanayohusiana na Mwaka Mpya kwa Wahindu.

"Wamenitaarifu kwamba watu 79 wamepoteza maisha," Oommen Chandy, kiongozi wa serikali ya jimbo hilo la kusini mwa India amekiambia kituo cha runinga cha NDTV. Awali ilisemekana kuwa watu 50 ndio walipoteza maisha.

Maafisa wa Zima Moto na askari polisi walikua wakikabiliana na moto huo usiku mzima katika hekalu hiyo inayopatikana katika wilaya ya Kollam, huku wakiwaokoa wahanga.

Picha zilizorushwa kwenye televisheni zimeonyesha mfululizo wa milipuko mikubwa na mwoshi mkubwa, pamoja na majeruhi wakiwasili katika hospitali za eneo hilo. moto ulianza baada ya 09:00 Alfajiri (sawa na saa 3:30 usiku saa za kimataifa Jumamosi hii).

Ajali za moto na mikanyagano hutokea mara nyingi katika mahekalu na wakati wa matukio ya kidini nchini India, kwa sababu hasa ya hatua dhaifu za usalama na viwango vya usalama visio kuwa thabiti.

"Hali kwa sasa imedhibitiwa," Waziri wa Mambo ya Ndani wa jimbo la Kerala, Ramesh Chennithala, amekiambia kituo cha runinga cha NDT.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.