Pata taarifa kuu
AZERBAIJAN-ARMENIA-MAPIGANO

Azebaijan: mapigano yaendelea Karabakh

Jumapili hii, Aprili 3, 2016, mapigano yameendelea katika eneo Karabakh katika jimbo la Caucasus Kusini, licha ya Azerbaijan kutangaza kusitisha mapigano.

Ndege aina ya Mi-24 ya Azerbaijani "iliyoanguka", ambayo ilipigwa picha na vikosi vya waasi wa  Nagorno-Karabakh, Aprili 2, 2016.
Ndege aina ya Mi-24 ya Azerbaijani "iliyoanguka", ambayo ilipigwa picha na vikosi vya waasi wa Nagorno-Karabakh, Aprili 2, 2016. Nagorno Karabakh Republic Defence Ministry / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mapigano, ambayo yalianza usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi, kati ya vikosi vya Azerbaijan na Armenia yamesababisha vifo vya watu wasiopungua thelathini.

Uturuki, mshirika wa karibu wa Baku, imeshutumu "uchokozi" wa Armenia, na imeitaka jumuiya ya kimataifa kujihusisha zaidi katika kutatua mgogoro huu.

Azerbaijan imetangaza Jumapili kuwa inasitisha mapigano katika eneo la Karabakh, ambapo yalizuka mwishoni mwa wiki hii mapigano muhimu zaidi tangu mwaka 1994 na mwisho wa vita viliotokea mwaka 1988 viliogharimu maisha ya watu 30 000 na kusababisha mamia ya maelfu ya wakimbizi wengi wao wakiwa watu kutoka jamii ya Waazeri. Lakini Baku (serikali ya Azerbaijan) imeongeza kwamba vikosi vya vyake vya jeshi vitaimarisha ulinzi katika ngome ziliotekwa, na kuwa vitajibu wakati wowote vitakaposhambuliwa.

Mbali na tangazo hilo, hata hivyo, msemaji wa waasi eneo la Karabakh lililojitenga, ambalo linaungwa mkono na Yerevan tangu kudhibitiwa kwa eneo hili wakati wa vita, amejibu kuwa "mapigano muhimu" yalikua bado hayajakoma, akitoa mfano wa "maeneo ya kusini na kaskazini ya mpaka". Kwa hiyo ni muhimu kwa kuwa makini kwa mabadiliko ya hali inayojiri katika masaa yajayo.

Jumamosi, Rais wa Urusi amesema kufuatia kuzuka kwa uhasama huo, huku akijaribu kuzitaka pande hizi mbili kusitisha mapigano. wakati huo huo Ankara imechukua msimamo wake katika neema ya Azerbaijan. Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki aliyataja mapigano hayo kama "shambulizi la Armenia", kabla ya kutoa wito kwa Yerevan kutangaza kusitisha mapigano.

Rais Recep Tayyip Erdogan pia alizungumza, amearifu mwandishi wetu katika mji wa Istanbul, Alexandre Billet. Amehakika kwamba Uturuki upande wa Azerbaijan "hadi mwisho". Na kuomba "kwa ushindi" wa wananchi wa Azerbaijan, ambao ni "ndugu zetu," amesema Rais wa Uturuki. Erdogan pia amekosoa, hasa, Jumuiya inayohusika na kutatua migogoro (OSCE), inayoongozwa na Ufaransa, Urusi na Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.