Pata taarifa kuu
BURMA-SIASA

Burma: chama cha Aung San Suu Kyi champendekeza Htin Kyaw

Aung San Suu Kyi ameachana rasmi Alhamisi hii na matarajio yake ya kuwa rais na kumpendekeza mmoja wa washirika wake wa karibu kuwa rais katika nafasi yake.

Htin Kyaw (kushoto) na Aung San Suu Kyi, siku ya kuachiliwa huru kwa Mama wa Rangoon, Novemba 13, 2010.
Htin Kyaw (kushoto) na Aung San Suu Kyi, siku ya kuachiliwa huru kwa Mama wa Rangoon, Novemba 13, 2010. STR/AFP
Matangazo ya kibiashara

"Napenda kumpendekeza Htin Kyaw kwa niaba ya NLD," amesema mbele ya Bunge Khin San Hlaing, Mbunge wa chama cha NLD cha Aung San Suu Kyi.

Aung San Suu Kyi hawezi kushikilia, angalau kwa muhula huu - kiti cha urais kwa sababu ya Ibara ya Katiba iliyowekwa na utawala wa kijeshi, ambayo inazuia kushikilia kiti cha urais kwa mtu yeyote ambaye ana watoto wenye uraia wa kigeni, hali ambayo inamkuta Aung San Suu Kyi, ambaye ana watoto wawili wenye uraia wa Uingereza.

Lakini mpaka Alhamisi asubuhi, wafuasi wake walikuwa na matumaini ambayo yangewashangaza wengi ya Mama maarufu wa Rangoon mwenyewe kushikilia kiti cha urais.

Kwa miezi kadhaa, mazungumzo yenye mantiki hiyo pamoja na wanajeshi vigogo yaliendelea, bila mafanikio. Kutokana na ukimya uliokuwepo tangu wakati huo, uvumi ulienea kote Burma kwamba daktari wa Aung San Suu Kyi au msaidizi wake ndio huenda mmoja kati ya wawili hao wangelishikilia kiti cha urais nchini Burma.

Siku hizi, jina la Htin Kyaw, mwenye umri wa miaka 69, limekua likirejea mara kwa mara midomoni mwa raia wa Burma.

Htin Kyaw, ni mwanauchumi na mtoto wa mwandishi na mshairi maarufu wa Burma na rafiki wa utotoni wa Aung San Suu Kyi. Alikua mara kwa mara dereva binafsi wa Aung San Suu Kyi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.