Pata taarifa kuu
INDONESIA-TSUNAMI-USALAMA

Indonesia: serikali yaonya kutokea kwa tsunami

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.8 richter katika Bahari ya Hindi limepiga Jumatano hii katika kisiwa cha Sumatra magharibi mwa Indonesia, eneo lililokumbwa na kuharibiwa na tetemeko la ardhi mwaka 2004. Serikali imetoa onyo kwa kutokea kwa tsunami.

Maelfu ya raia wa Indonesia wakifanya ibada katika Msikiti Mkuu wa Banda Aceh tarehe 26 Desemba 2014, wakiwakumbuka waathirika wa tsunami ya mwaka 2004.
Maelfu ya raia wa Indonesia wakifanya ibada katika Msikiti Mkuu wa Banda Aceh tarehe 26 Desemba 2014, wakiwakumbuka waathirika wa tsunami ya mwaka 2004. REUTERS/Beawiharta
Matangazo ya kibiashara

Tetemeko hili limetokea saa 12:50 jioni saa za Indonesia (sawa na saa 6:50 saa za kimataifa) kwenye kilomita 24 za kina na kitovu kilikuwa kilomita kadhaa na visiwa vya Mentawi, eneo dogo kusini magharibi mwa Sumatra, kitengo cha utabiri wa mambo ya hewa cha Marekani (USGS)kimesema.

USGS, hata hivyo, imesema katika tovuti yake kwamba "uwezekano wa majeruhi na uharibifu" haukua kwa kiwango kikubwa.

Idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini Indonesia (BMKG) imetoa onyo kwa kutokea tsunami katika sehemu mbalimbali za Sumatra, hususan Sumatra ya Kaskazini na Sumatra ya Magharibi, pamoja na Aceh, Bengkulu na Lampung.

Mji ulio karibu na Sumatra ni Padang. Mwandishi wa habari wa Shirika la habari la Ufaransa la AFP katika mjihuo amearifu kwamba tetemeko kubwa la ardhi limesikika kwa sekunde chache na wakazi waliondoka haraka katika nyumba zao.

Tukio hili limesababisha hali ya wasiwasi katika mitaa, kwa mujibu wa chanzo hicho.

Kiongozi wa Idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini Indonesia (BMKG), Andi Eka Sakya, hata hivyo, amesema kwenye televisheni moja nchini humo TV One: "Kwa sasa hatuna taarifa kuhusu uharibifu mkubwa."

Jinsi tetemeko la ardhi lilivyosababisha tsunami ya 2004.
Jinsi tetemeko la ardhi lilivyosababisha tsunami ya 2004. Creative commons/RobinL

Kwa upande wake, Australia pia imetoa onyo kwa kutokea kwa tsunami katika mikoa ya magharibi ya Nchi-bara, jirani ya Indonesia, lakini baadae onyo hilo lilifutwa.

Indonesia iko kwenye "eneo la hatari" la Pasifiki, ambapo mgongano wa mihimili ya tectonic husababisha matetemeko ya mara kwa mara na mlipuko muhimu wa volkano.

Mwaka 2004, tetemeko kubwa, kaskazini magharibi mwa Indonesia, lilisababisha tsunami kubwa, lililoua watu zaidi ya 170,000 nchini Indonesia na mamia ya maelfu zaidi katika nchi nyingine kadhaa za Bahari ya Hindi.

Tangu tsunami ya mwaka 2004, hatua za kuzuia au kukinga hali hiyo zimechukuliwa duniani kote.
Tangu tsunami ya mwaka 2004, hatua za kuzuia au kukinga hali hiyo zimechukuliwa duniani kote. Creative commons/debaird

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.