Pata taarifa kuu
INDONESIA-IS-MASHAMBULIZI

Indonesia: watu 7 wauawa katika mashambulizi Jakarta

Watu wasiopungua saba, ikiwa ni pamoja na washambuliaji watano, wameuawa Alhamisi hii katika mashambulizi, ambayo yamezua hali kubwa ya sintofahamu mjini Jakarta, na kusababisha hofu kwa raia kwamba kundi la Islamic State huenda limeanzisha harakati zake katika visiwa vya kusini mashariki mwa Asia.

Askari polisi wa Indonesiawatenda eneo la usalama mbele ya mgahawa wa Starbucks baada ya mashambulizi katika mji wa Jakarta, Januari 14, 2016.
Askari polisi wa Indonesiawatenda eneo la usalama mbele ya mgahawa wa Starbucks baada ya mashambulizi katika mji wa Jakarta, Januari 14, 2016. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya washambuliaji wawili wa kujitoa mhanga wamejilipua katika eneo la kati mwa mji mkuu lenye Ofisi nyingi za mashirika ya Umoja wa Mataifa na balozi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ubalozi wa Ufaransa, ambapo milipuko imesikika.

Washambuliaji ambao wamelenga mgahawa wa Starbucks, hawajulikani, lakini rais, Joko Widodo, ameyataja mashambulizi hayo kama vitendo vya "kigaidi" na polisi imetangaza kuwa kundi lenye mafungamano na Islamic State (IS) linashukiwa kutekeleza mashambulizi hayo.

Serikali ya Indonesia ilitangaza wiki chache zilizopita kwamba ilivunja shambulio la kujitoa mhanga lililokua limepangwa na magaidi wenye msimamo mkali, baadhi wakiwa na uhusiano na kundi la IS.

"Magaidi watano wameuawa", Waziri wa usalama wa Indonesia, Luhut panjaitan, amewaambia waandishi wa habari Alhamisi hii mchana, akiongeza kuwa raia mmoja wa Indonesia na mwengine kutoka Uholanzi wameuawa katika mashambulizi hayo.

Ubalozi wa Uholanzi haujaithibitisha taarifa hii, lakini ukisema kwamba mmoja wa raia wake amejeruhiwa na amelazwa hospitalini.

Polisi imesema kuwa imedhibiti hali ya mambo na washambuliaji wote wameangamizwa. "Hali kwa sasa imedhibitiwa", amesema Muhammad Iqbal, msemaji wa polisi ya mji wa Jakarta.

Hata hivyo Muhammad Iqbal pia amesema kuwa askari polisi watano, raia mmoja wa kigeni na raia wanne wa Indonesia wamejeruhiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.