Pata taarifa kuu
BANGLADESH-MAUAJI-SHERIA-HAKI

Rais wa Bangladesh afutilia mbali msamaha kwa wapinzani walio hukumiwa kifo

Rais wa Bangladesh Abdul Hamid amefutilia mbali ombi la msamaha wa viongozi wawili wa upinzani waliohukumiwa adhabu ya kifo kutokana na kuhusika kwao kwa vita vya uhuru vya mwaka 1971, Waziri wa mambo ya ndani amesema.

Rais wa Bangladesh Abdul Hamid katika mji wa Dhaka, Juni 7, 2015.
Rais wa Bangladesh Abdul Hamid katika mji wa Dhaka, Juni 7, 2015. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

"Rais amefutilia mbali maombi yao ya msamaha", waziri, Asaduzzaman Khan, ameliambia shirika la habari la AFP, na kuongeza kwamba viongozi walikuwa wakiandaa kutekeleza adhabu hiyo ya kifo..

Mamlaka ya magereza iliziomba familia za Ali Ahsan Muhammad Mujahid na Salahuddin Quader Chowdhury kuja kukutana nao katika gereza kuu la Dhaka, kauli hiyo inaonyesha kuwa wafungwa hao wanapaswa kunyongwa katika masaa yajayo.

"Mamlaka ya gereza imetuita kwenda kukutana na baba yetu. Hii ni dhahiri mazungumzo yetu ya mwisho na baba yetu", Ali Ahmad Marbrur mwanaye Mujahid, ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP. Mamia ya askari polisi kwamezunguka eneo la gerezani.

Hojatul Islam, mwanasheria wa Salahuddin Quader Chowdhury, amesema familia yake ilikuwa tayari kuwasili katika gereza kukutana naye.

Mujahid, mwenye umri wa miaka 67, anayetuhumiwa mauaji ya wasomi maarufu, alihukumiwa kifo kwa uhalifu wa kivita. ni kiongozi wa pili wa chama muhimu cha Kiislam nchini humo, Jaamat-e-Islami.

Chowdhury, mwenye umri wa miaka 66, alihukumiwa kwa kosa la mauaji yaliyofanywa wakati wa vita vya uhuru wa 1971, ikiwa ni pamoja na mauaji ya kimbari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.