Pata taarifa kuu
BURMA-UCHAGUZI-SIASA

Burma: jeshi laahadi kushirikiana na serikali mpya

Chama cha LND cha Aung San Suu Kyi kimedai ushindi mkubwa katika uchaguzi wa wabunge wa Jumapili iliyopita. Tume ya uchaguzi imethibitisha kuwa chama cha LND cha kiongozi wa upinzani Aung San Suu Kyi kimeshinda viti 211 kwa jumla ya viti 230.

Picha hii imetolewa na ofisi ya mkuu wa majeshi kwa vyombo vya habari, jenerali Min Aung Hlaing akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura katika mji mkuu, Novemba 8, 2015.
Picha hii imetolewa na ofisi ya mkuu wa majeshi kwa vyombo vya habari, jenerali Min Aung Hlaing akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura katika mji mkuu, Novemba 8, 2015. AFP PHOTO / COMMANDER-IN-CHIEF OFFICE
Matangazo ya kibiashara

Chama cha majenerali wa zamani kilio madarakani kimekiri kushindwa na kuhakikisha kikotayari kukabidhi madaraka kwa amani.

"Wananchi wameonyesha nia yao katika uchaguzi", Suu Kyi ameandika katika barua aliowatumia mkuu wa majeshi Min Aung Hlaing, Rais Thein Sein na Spika wa bunge mwenye ushawishi mkubwa, Shwe Mann.

Aung San Suu Kyi amekiri kwamba uchaguzi mkuu uliofanyika Jumapili nchini humo haukuwa huru lakini ulikuwa wa haki, huku akiwapongeza watu wa Myanmar kwa kujitokeza kwa uwingi kushiriki uchaguzi huo.

Jeshi limemkaribisha Aung San Suu Kyi. Limekubali ushindi wa chama cha upinzani. Mkuu wa vikosi vya kijeshi amekubali kukutana na Aung San Suu Kyi. Kabla ya uchaguzi wa Jumapili, jenerali Aung Min Hlaing mara zote alikataa kukutana kwa mazungumzo nakiongozi huyo wa upinzani. Wakati huu hawezi kupuuza matokeo ya uchaguzi huo. Matokeo wazi tangu tume ya uchaguzi kuthibitisha kuwa chama cha LND kimepata viti vya kutosha katika baraza la Bunge kwa kumteua Makamu wa rais.

"Jeshi litafanya kilio chini ya uwezi wake, kwa kushirikiana na serikali mpya", amesema jenerali Min Aung Hlaing wakati wa hotuba yake mbele ya viongozi wa juu wa kijeshi nchini Burma, huku akiwatolea wito wanajeshi "kutii na kuwa na nidhamu."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.