Pata taarifa kuu
RIADHA-MCHEZO

Mabingwa wa dunia wa Riadha: Usain Bolt bado anaongoza

Usain Bolt ametunukiwa Jumapili Agosti 23 taji la tatu la bingwa wa dunia katika mbio za mita 100. Raia huyo wa Jamaica ambaye alipata matatizo msimu huu alikua ana imani kuwa raia wa Marekani Justin Gatlin, ambaye kila mara anakimbia kwa kasi ndiye atanyakua ubingwa.

Raia wa Jamaica, Usain Bolt, anaadhimisha taji lake la tatu la dunia katika mbio za mita 100, Agosti 23, 2015, Pékin.
Raia wa Jamaica, Usain Bolt, anaadhimisha taji lake la tatu la dunia katika mbio za mita 100, Agosti 23, 2015, Pékin. REUTERS/Lucy Nicholson
Matangazo ya kibiashara

Usain Bolt amejikuta hatimaye katika hatua ya fainali akikabiliana katika mashindano hayo na Justin Gattin.

Usain Bolt bado anaongoza hata hivyo katika mashindano ya Riadha. Licha ya majeruhi yaliomkabili msimu wake. Licha ya muda unavyokwenda na umri wake wa miaka 29 aliosheherekea Ijumaa wiki hii. Mjini Beijing, mwaka 2015 na 2008 katika Michezo ya Olimpiki, Usain Bolt bado anaongoza.

Justin Gatlin alikuwa bado na imani ya kushinda. Raia huyo wa Marekani alikuwa akiongoza kwa mita 80. Baada ya kushindwa tangu msimu uliopita, alikuwa anakaribia kushinda na kuwa bingwa wa dunia miaka kumi baadaye. Ila kwa kuwa Bolt bado anaongoza katika mashindano hayo ya Riadha, Justin Gattin ameonekana kuangukia pua na kupoteza nafasi hiyo. Katika pambano hilo, Justin Gattin ndiye aliendelea kuonekana kuwa mtu mwenye ufanisi mkubwa. Akikimbia sentimita baada sentimita, Jusin Gattin alijikuta anashindwa kufanya vizuri katika hatua ya mwisho, baada ya mikono yake kwenda pande zote.

Katika sekunde 9.79, Usain Bolt ameweza muda wake bora wa mwaka katika siku kama hii. Kama kawaida, radi inapiga wakati unaotakiwa. " Hii ni dhahiri mbio zangu zimekua ngumu sana kwa kutetea taji hili. Justin (Gatlin) alikimbia vizuri sana kwa mwaka wote huu na kocha wangu na mimi tulifahamu kadri miaka ilivyokua ikienda kwamba Justin Gattin ataweza kuongeza kiwango chake katika michuano ya mbio za Riadha. Nilijua kwamba kama ntakuja hapa kushinda, nitakua bingwa wa mashindano haya kwa mara nyingine tena. Mimi ninajiamini. Nilikabiliwa na mambo mengi msimu huu. Nilikuwa na heka heka, kwa hivyo kwangu mimi, kufanikiwa kwa kila jambo kwa wakati muafaka, ni ushindi mkubwa ", amesema bingwa huyo wa mashindano ya Riadha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.