Pata taarifa kuu
TAIWAN-AJALI-USALAMA

Taiwan: ndege yaanguka mtoni ikiwa na abiria 58

Baada ya ajali ya ndege iliyogharimu maisha ya abiria 54 mwezi Julai mwaka uliyopita nchini Taiwan, ndege nyingine ya shirika la ndege la TransAsia imeanguka asubuhi mapema Jumatano wiki hii katika mji mkuu wa nchi hiyo, Taipei.

Ndege ya shirika la ndege la Taiwan TransAsia ikiangika mtoni ikiwa na abiria, Februari 4 mwaka 2014.
Ndege ya shirika la ndege la Taiwan TransAsia ikiangika mtoni ikiwa na abiria, Februari 4 mwaka 2014. Capture d'écran Youtube
Matangazo ya kibiashara

Kwa jumla ya abiria 58 waliokua ndani ya ndege hio, 11 wanashukiwa kufariki, takribani 18 wameokolewa, huku 30 wakiwa bado wamenasa katika ndege hiyo.

Ngede hiyo ilikua ikitokea katika uwanja ndege wa Songshan mjini Taipei, ikielekea katika kisiwa cha Kinmen kwenye mwambao wa China. Muda mchache baada ya kuruka, kwenye saa tano asubuhi (saa za Taiwan), ndege hiyo ilijigonga kwenye daraja kabla ya kuanguka katika mto Keelung, kwa sababu ambazo bado hazojajulikana.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya usafiri wa anga, ndege hiyo ilikuwa imebeba watu 58 ikiwa ni pamoja na wafanyakazi watano. Wakati huu, abiria 18 waliokolewa na kusafirishwa hospitalini, amesema afisa wa shughuli za uokozi kwenye mtandao.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa AFP, watu kumi na moja wamefariki na thelathini wengine zaidi ya thelathini bado wamenasa katika ndege, wakati ambao shughuli za uokozi zikiendelea ili kuwaondoa abaria ambao bado wamenasa katika ndege hiyo ambayo inaendelea kuzama.

Hii ni ajali ya pili katika kipindi cha miezi saba kwa shirika la ndege la Taiwan. Julai 23, ndege ya shirika la la ndege la Taiwan TransAsia ilianguka katika kisiwa cha Penghu, magharibi mwa Taiwan, wakati dhoruba Matmo ilikua ikipiga katika ukanda huo. Kwa jumla ya abiria 58, 48 walifariki, ikiwa ni pamoja na raia wawili wa Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.