Pata taarifa kuu
BURMA-MAREKANI-Demokrasia-Madeuzi-Siasa

Burma: Obama ataka mageuzi na mfumo wa kidemokrasia

Rais wa Marekani Barack Obama amekuna kwa mazungumzo leo Ijumaa novemba 14 mjini Yangon na kiongozi wa upinzani nchini Burma, Aung San Suu Kyi, wakati taifa hilo likielekea katika uchaguzi wa mwaka ujao na kutokuwa na uhakika juu ya mwelekeo wa mageuzi.

Katika mkutano wa kilele wa Asean, Barack Obama amekutana na wabunge kadhaa, ikiwa ni pamoja na kiongozi wa upinzani nchini Burma, Aung San Suu Kyi, Novemba 13 mwaka 2014.
Katika mkutano wa kilele wa Asean, Barack Obama amekutana na wabunge kadhaa, ikiwa ni pamoja na kiongozi wa upinzani nchini Burma, Aung San Suu Kyi, Novemba 13 mwaka 2014. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Obama amemkuta kiongozi huyo wa upinzani nchini Burma nyumbani kwake ambapo anazuiliwa kifungo cha nyumbani.

Obama na Suu Kyi wamesema mageuzi zaidi yenye mfumo wa kidemokrasia yanapaswa kufanyika, ili raia kutoka makundi mbalimbali wanaohitashi kushiriki uchaguzi wasiendelei kubanwa na utawala.

Chama cha Suu Kyi cha National League for Democracy (NLD) kinatarajiwa kwa kiasi kikubwa kujikusanyia kura nyingi katika uchaguzi wa mwaka 2015, lakini kiongozi wake anazuiwa kuwania madaraka na kifungu cha kikatiba.

Obama amejielekeza Yangon,akitokea kwenye mazungumzo baada ya mkutano wa Asia Mashariki uliofanyika Naypyidaw na mshirika wake wa Myanmar Thein Sein, ambaye amesimamia mageuzi tangu mwaka 2011.

Rais wa Marekani Barack Obama ametoa wito wa kuendelea na mageuzi zaidi nchini Burma. Wito huo aliutoa katika mkutano wa kilele wa Asean uliyofanyika katika mji mkuu wa Burma, wakati wa mkutano na wabunge kadhaa, ikiwa ni pamoja na mpinzani akiwa pia mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, Aung San Suu Kyi, ambae amekutana naye kwa mazungumzo Ijumaa Novemba 14 mjini Yangon.

Marekani ilichangia kwa kupatikana kwa mageuzi yenye mfumo wa kidemokrasia nchini Burma. Hata hivyo rais Barack Obama amesema hatokubali mchakato huo utawaliwe na ukiritimba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.