rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Pakistani Marekani Al Qaeda Osama Bin Laden

Imechapishwa • Imehaririwa

Marekani yatangaza dola 10,000 kumsaka Saeed, mahakama yawahukumu wajane wa Osama

media
RFI/Anthony Terrade

Marekani imetangaza zawadi ya kitita cha dola 10,000 kwa atakayefanikisha kukamatwa kwa Hafiz Saeed ambaye ni kiongozi wa kundi kigaidi cha Pakistan ambacho kimekuwa kikituhumiwa na India kuwa kinafanya mashambulizi kadhaa nchini humo.


Serikali ya Marekani imesema imeamua kufanya hivyo kwa kiongozi huyo anatuhumiwa kupanga mashambulizi ya mjini Mumbai mwaka 2008 na amekuwa akisaidia kuhujumiwa kwa majeshi ya NATO yaliyoko Afghanistan.

Wakati huohuo mahakama nchini Pakistan imewahukumu Wajane watatu wa Kiongozi wa zamani wa Mtandao wa Al Qaeda Duniani pamoja na watoto wawili wakubwa wa Osama Bin Laden kifungo cha siku arobaini na tano jela na kisha kufukuzwa kutokana na kuingia kinyume cha sheria katika nchi hiyo.

Uamuzi wa Mahakama umekuja baada ya ushahidi kudhihirisha wajane hao watatu pamoja na watoto wao ambao ni raia wa Sauri Arabia na Yemeni walikuwa wanaishi kinyume cha katika nchi hiyo katika Mji wa Abbottabad.

Mwanasheria wa Familia ya Osama, Muhammad Aamir amekubaliana na uamuzi huo na kusema katika kipindi cha majuma mawili watakuwa wameshakamilisha hatua zote za watu hao kuondoka Pakistan.