Pata taarifa kuu
INDIA

Mwanaharakati Anna Hazare aachiwa na sasa kufunga kwa siku 15

Mwanaharakati Mkongwe nchini India ambaye amekuwa kinara katika kupambana na vita dhidi ya ulaji wa rushwa Anna Hazare ameondolewa mahabusu mapema leo baada ya kukubaliana na polisi atafunga kwa kipindi cha siku kumi na tano.

Mwanaharakati Mkongwe Nchini India Anna Hazare mara baada ya kukamatwa na Polisi
Mwanaharakati Mkongwe Nchini India Anna Hazare mara baada ya kukamatwa na Polisi
Matangazo ya kibiashara

Hazare alikamatwa siku ya jumanne asubuhi baada ya kusema kuwa atafunga hadi atakapofikwa na mauti akishinikiza serikali kuridhia mapendekezo yake ya namna ya kushughulikia suala la rushwa.

Hazare mwenye umri wa miaka sabini na minne anatarajiwa kuanza kufunga baadaye hii leo kuonesha hisia alizonazo katika kukabiliana na vitendo vya rushwa ambavyo vimezidi kuota mizizi katika nchi hiyo.

Maelfu ya wananchi wamejitokeza kumlaki Hazare ambaye hapo jana alikataa kutoka mahabusu alipokuwa anashikiliwa kwa madai ataendelea na uamuzi wake wa kufunga hadi afe au serikali itekeleza mapendekezo yake.

Msemaji wa Hazare, Aswathi Muralidharan amesema baada ya mazungumzo ambayo yamefanywa na polisi ndiyo Mwanaharakati huyo akaamua kupunguza siku za kufunga toka siku thelathini hadi kumi na tano.

Wafuasi wa Hazare wamejitokeza katika eneo la Ramlila Maidan kuungana na Kiongozi wao baada ya kuachiwa na sasa ataendelea na kampeni yake ya kuishinikiza serikali kupambana vilivyo na vitendo vya rushwa vinavyozidi kushamiri.

00:25

Waziri Mkuu wa India Manmohan Singh Akihutubia Bunge Juu ya Kukamatwa kwa Anna Hazare

Tayari Waziri Mkuu wa India Manmohan Singh jana aliliambia Bunge kuwa kitendo ambacho kimefanywa na Hazare hakiwezi kuvumiliwa kwa kuwa kinachangia kutishia uwepo wa demokrasia katika nchi hiyo.

Singh ameendelea kusisitiza kuwa serikali yake itaendelea kupambana na vitendo vya rushwa wakati huu ambapo ni siku nne zimepita baada ya nchi hiyo kusherehekea kumbukumbu ya siku yao ya Uhuru.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.