Pata taarifa kuu
Chile

Polisi nchini Chile wapambana na waandamanaji

Polisi nchini Chile wamepambana na maelfu ya waandamanaji katika mji mkuu wa nchi hiyo santiago ambapo watu kadhaa wanashikiliwa na polisi kwa kushiriki kuandaa maandamano hayo yaliyopigwa marufuku na serikali.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Wanafunzi, wazazi pamoja na walimu waliingia mtaani siku ya jumanne wakipinga mfumo wa elimu uliotangazwa na serikali ambapo wazazi watalazimika kuchangia huku shule nyingi zikimilikiwa na serikali za mitaa kitu ambacho wananchi hao wanadai kimeleta ubaguzi katika utolewaji wa elimu.

Polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi na risasi za mpira kuwatawanya waandamanaji hao ambao wameapa kuendelea na maandamano ya nchi nzima wakisisitiza kutokaa meza moja na serikali ya rais Sebastian Pinera mpaka pale atabadili mfumo huo wa elimu.

Haya ni maandamano ya pili kufanywa na wananchi ndani ya wiki moja kufuatia juma lililopita kufanyika maandamano kama hayo na watu zaidi ya 60 kushikiliwa na polisi.
Β 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.