Pata taarifa kuu
Misri

Mahakimu nchini Misri wachunguzwa baada ya kulikososa jeshi

Wizara ya sheria nchini Misri inawachunguza mahakimu watatu waliokosoa kesi za raia kusikilizwa katika mahakama za kijeshi, vyombo vya habari vya nchi hiyo vimethibitisha. 

Askari mmoja wa Jeshi la Misri akiwasiliana na waandamanaji jijini Cairo, Misri.
Askari mmoja wa Jeshi la Misri akiwasiliana na waandamanaji jijini Cairo, Misri.
Matangazo ya kibiashara

Majaji hao walinukukuliwa na vyombo vya habari vya Misri wakionesha hofu yao, endapo haki itatendeka kwa kesi za kiraia zisikilizwa katika mahakama za kijeshi .

Wizara ya sheria inasema hatua hiyo imekuja baada ya majaji hao, kuzungumza na vyombo vya habari bila ruhusa huku wenyewe wakisisitiza kuwa hawahitaji ruhusa ili kuelezea mawazo yao.

Uhuru wa kutoa maoni mojawapo ya haki za binadamu, zinazotambuliwa na Umoja wa Mataifa.

Tangu Rais Hosni Mubarak aondolewe madarakani mwezi wa pili, mwaka huu mashirika ya kutetea haki za binadamu yanapasha kuwa jeshi linalotawala Misri, limeshasikiliza kesi kama hizo zaidi ya elfu kumi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.