Pata taarifa kuu
BOLIVIA-UCHAGUZI-SIASA

Bolivia: Evo Morales marufuku kuwania katika Uchaguzi wa maseneta

Rais wa zamani wa Bolivia Evo Morales amepigwa marufuku kuwania katika uchaguzi wa maseneti, uamuzi ambao umechukuliwa taasisi kuu ya uchaguzi nchini Bolivia.

Rais wa zamani wa Bolivia Evo Morales, aliyejiuzulu, katika mkutano wa waandishi wa habari Novemba 20, 2019 huko Mexico, ambayo ilimpa hifadhi ya ukimbizi.
Rais wa zamani wa Bolivia Evo Morales, aliyejiuzulu, katika mkutano wa waandishi wa habari Novemba 20, 2019 huko Mexico, ambayo ilimpa hifadhi ya ukimbizi. PEDRO PARDO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inahatarisha kurudi kwake kisiasa baada ya kujiuzulu mwezi Novemba.

Mahakama Kuu ya Uchaguzi ya Bolivia (TSE) imebaini kwamba Evo Morales hajatimiza wajibu wa "makazi ya kudumu" nchini Bolivia.

Evo Morales aliondoka Bolivia kwenda Mexico baada ya kujiuzulu mwezi Novemba, baada ya wiki kadhaa za maandamano dhidi yake na chini ya shinikizo kutoka kwa vikosi vya jeshi, kufuatia uchaguzi wa urais uliokumbwa na utata. Kisha akakimbilia Argentina.

Uamuzi wa Mahakama "ni pigo dhidi ya demokrasia. Wajumbe (wa mahakama hii) wanajua kuwa ninatimiza masharti ya kuwa mgombea. Malengo yao ni kukifuta kabisa chama cha MAS", amebaini Bwana Morales kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Kwa upande wake, mpinzani wake mkuu, Rais wa zamani Carlos Mesa amekaribisha uamuzi wa mahakama, akisema, "sheria na Katiba vimetumiwa kwa usahihi". Evo Morales "anapaswa kuelewa kuwa hawezi tena kutumia sheria kulingana na masilahi yake," ameongeza.

Chama cha Bw. Morales, MAS, hata hivyo kitawakilishwa katika uchaguzi wa urais. Waziri wa zamani wa Uchumi, Luis Arce, amekubaliwa na Mahakama Kuu ya Uchaguzi kuwania katika uchaguzi wa urais, Mkuu wa mahakama hiyo Salvador Romero alisema Alhamisi katika mkutano na waandishi wa habari.

Aliteuliwa rasmi kupeperusha bendera ya chama cha MAS Februari 9, 2020.

Waziri wa zamani wa Uchumi, Luis Arce, amekubaliwa na Mahakama Kuu ya Uchaguzi kuwania katika uchaguzi wa urais.
Waziri wa zamani wa Uchumi, Luis Arce, amekubaliwa na Mahakama Kuu ya Uchaguzi kuwania katika uchaguzi wa urais. MARIANA GREIF
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.