Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP

Bunge la seneti la muondolea hatia rais Trump

Rais wa Marekani Donald Trump amesafishwa na bunge la seneti katika kesi iliyokuwa ikimkabili, hatua inayomaliza rasmi juhudu za bunge la Congress kutaka kumuondoa madarakani kabla ya uchaguzi wa mwezi Novemba.

Rais wa Marekani Donald Trump akihutubia wabunge katika hotuba yake kwa taifa, 4/02/2020.
Rais wa Marekani Donald Trump akihutubia wabunge katika hotuba yake kwa taifa, 4/02/2020. REUTERS/Leah Millis
Matangazo ya kibiashara

Bunge la seneti linalokaliwa na wabunge wengi wa chama cha Repuboican, lilipiga kura 52 kwa 48 katika makosa ya matumizi mabaya ya ofisi na kura 53 kwa 47 katika makosa ya kulidharau bunge.

Wabunge wa Democrats walimfungulia mashtaka rais Trump mwezi Desemba mwaka jana wakimtuhumu kumshinikiza rais wa Ukraine kufanya uchunguzi dhidi ya hasimu wake wa kisiasa Joe Biden.

Wabunge wa Seneti wakati wa moja ya mijadala kuhusu kumuondoa madarakani Donald Trump
Wabunge wa Seneti wakati wa moja ya mijadala kuhusu kumuondoa madarakani Donald Trump REUTERS/U.S. Senate TV/Handout via Reuters

Kwa kura hii sasa ina maanisha kuwa rais Trump ataendelea kusalia madarakani.

Katika uchaguzi mkuu wa mwezi Novemba mwaka huu rais Trump atakuwa rais wa kwanza kuomba kura achaguliwe tena kuongoza taifa hilo.

Katika kura ya kihistoria iliyofanyika usiku wa Jumatano, bunge la seneti liliamua kutokumuondoa madarakani rais wa 45 wa Marekani katika mashtaka yaliyotokana na namna alivyoshughulikia suala la misaada ya kijeshi ya Ukraine.

Ikiwa rais Trump angekutwa na hatia ya makosa yaliyokuwa yakimkabili, basi angelazimika kukabidhi madaraka yake kwa makamu wa rais Mike Pence.

Wabunge wa Democrats ambao wanaongoza bunge la Congress waliidhinisha hati ya mashtaka dhidi ya Trump tarehe 18 Desemba.

Punde baada ya kura hiyo rais Trump aliandika kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Twitter, akiwashutumu wabunge wa Democrats kwa kutaka kumuondoa madarakani rais halali wa Marekani.

Hata kabla ya kura hii umaarufu wa rais Trump umeongezeka isivyo kawaida kwa mara ya kwanza na kufikia asilimia 49.

Wadadisi wa siasa wa Marekani wanasema njia pekee ya kumuondoa madarakani rais Trump ni kwa kupitia uchaguzi mkuu wa mwezi November.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.