Pata taarifa kuu
MAREKANI-ALENA-UCHUMI

Trump kutia saini kwenye mkataba wa biashara wa Amerika ya Kaskazini Jumatano

Rais wa Marekani, Donald Trump atatia saini kwenye mkataba mpya wa biashara huria kati ya Marekani, Mexico na Canada Januari 29, afisa mmoja wa serikali ya Marekani ameliambia shirika la habari la Reuters.

Rais wa Marekani Donald Trump.
Rais wa Marekani Donald Trump. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Nakala hiyo ilipitishwa na Bunge la Seneti kwa idadi kubwa mwezi huu, baada ya kupitishwa mwezi Desemba na Baraza la Wawakilishi.

Mkataba huo unaojulikana kwa jina la USMCA (United States-Mexico-Canada), unatarajiwa kuwa mkataba wa biashara huria wa Amerika ya Kaskazini (Alena).

Mkataba huo ulianza kutumika mnamo mwaka 1994 na ni wenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1,200 katika biashara ya kila mwaka, ikiwa ni pamoja na theluthi moja ya mauzo ya nje ya kilimo kutoka Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.