rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani Iran Donald Trump

Imechapishwa • Imehaririwa

Bunge lapitisha azimio la kuzuia hatua ya kijeshi ya Trump dhidi ya Iran

media
Azimio linamtaka rais Trump "kuacha kulitumia jeshi la Marekani" dhidi ya Iran mpaka apate kibali cha Baraza la Wawakilishi. Mark Wilson/Getty Images/AFP

Baraza la Wawakilishi linalodhibitiwa na chama cha Democratic limepitisha azimio siku ya Alhamisi ya kuzuia mamlaka ya Donald Trump kuzindua oparesheni za kijeshi dhidi ya Iran, nakala ambayo ni ishara lakini ni maudhi kwa rais Trump.


Kumhimiza Donald Trump "kusitisha" hatua zote za kijeshi dhidi ya Iran kwa kutoungwa mkono na Baraza la Congress, azimio hilo limepitishwa kwa kura 224 dhid ya 194.

Inaonekana kuwa azimio hilo litapelekwa mbele ya Bunge la Seneti, linalodhibitiwa na chama cha Republican ambalo linamuunga mkono kwa idadi kubwa ya wajumbe Donald Trump.

Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi. REUTERS/Kevin Lamarque

Azimio hilo linalenga kulipa Baraza la Congress nguvu ya kutoa kibali cha shambulio lolote dhidi ya Iran, isipokuwa pale tu patakapokuwa na shambulio la ghafla dhidi ya Marekani.

Kwa sasa hakuna upande kati ya Iran na Marekani ambao umetamka kuwa utaendelea na mashambulizi.