Pata taarifa kuu
MAREKANI-BOEING-USALAMA

Boeing yasitisha kwa muda kuzalisha ndege za 737 MAX kuanzia Januari

Kampuni ya Marekani ya kutengeneza ndege, Boeing, inaendelea kukumbwa na mgogoro mbaya zaidi katika historia yake na kutangaza kusitisha kuzalisha ndege za 737 MAX ifikapo Januari 2020.

Wafanyakazi wa kampuni ya Boeing wakitengeneza ndege ya 737 Max katika kiwanda cha Renton katika Jimbo la Washington nchini Marekani, Machi 23, 2019.
Wafanyakazi wa kampuni ya Boeing wakitengeneza ndege ya 737 Max katika kiwanda cha Renton katika Jimbo la Washington nchini Marekani, Machi 23, 2019. AFP Photos/Jason Redmond
Matangazo ya kibiashara

Ndege hiyo imepigwa marufuku kupaa tangu Machi 2019 baada ya ajali mbili mbaya za ndege za chapa hiyo.

Zaidi ya watu 300 walipoteza maisha wakati ndege mbili za 737 MAX zilipoanguka katika nchi za Indonesia na Ethiopia baada ya kuripoti matatizo katika mfumo wake mpya.

Kwa miaka 20, hii ni mara ya kwanza kampuni ya Boeing inalazimika kusitisha uzalishaji. Hatua hiyo itaanza kutumika vizuri kuanzia mwezi Januari 2020. Ilichukua siku mbili za majadiliano kwa bodi ya wakurugenzi ya kampuni hiyo huko Chicago na kufikia kuchukua hatua Jumatau Desemba 16, mwandishi wetu nchini Marekani, Éric de Salve, ameripoti.

Boeing imekua ikitumaini kuwa ndege hizo zitarejea tena angani kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Uchunguzi wa shirika la safari za ndege nchini Marekani ulionesha kuwa zinaweza kutokea ajali nyingine zaidi ya kumi na mbili za ndege za 737 MAX ikiwa hakuna mabadiliko yatakayofanyika kwenye muundo wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.