Pata taarifa kuu
CHILE-SIASA-USALAMA

Chile: Vurugu na maandamano vyanaendelea kwa siku 40 sasa

Waandamanaji nchini Chile wanaendelea kumiminika mitaani, siku 40 baada ya kuanza kwa maandamano makubwa zaidi ya kutaka mabadiliko ya kiuchumi na kujiuzulu kwa rais Sebastian Pinera.

Waandamanaji wakiweka vizuizi barabarani, Novemba 26, 2019.
Waandamanaji wakiweka vizuizi barabarani, Novemba 26, 2019. REUTERS/Jose Luis Saavedra
Matangazo ya kibiashara

Madai ya waandamnaji mpaka sasa hayajapatiwa ufumbuzi na serikali ya Chile.

Maelfu ya watu waliandamana tena Jumanne wiki hii katika mitaa ya Santiago wakiitikia wito uliotolewa na vyama vya wafanyakazi katika sekta ya umma, kwa mujibu a shirika la Habari la AFP.

Wimbi la maandamano lililoanza Oktoba 18 linaendelea katika hali ambayo imekuwa ya kawaida huko Santiago.

Kwa muda wa wiki kadhaa, ghadhabu ya raia wa Chile imeendelea kusambaa kama maandamano dhidi ya mfumo wa kijamii na kiuchumi ambao wengi wanahisi kuwa umewatenga, huku wakipata mapato ya chini na mafao, gharama ya juu ya matibabu na elimu na pengo kubwa kati ya matajiri na maskini.

Wataalamu wa masuala ya afya na makundi ya haki za binaadamu wanakadiria kuwa takribani watu 220 wamepata majeraha ya macho kwa kipindi cha mwezi mmoja wa maandamano.

Na ripoti mpya ya Shirika la Amnesty International, shirika ambalo lilifanya uchunguzi katika nchi hiyo ya kusini mwa Amerika, imeshutumu serikali ya Chile kuwadhuru waandamanaji makusudi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.