Pata taarifa kuu
BOLIVIA-SIASA-USALAMA

Hali ya wasiwasi yatanda Bolivia

Novemba 10, Evo Morales alijiuzulu baada ya wiki kadhaa za maandamano kupinga kuchaguliwa kwake tena katika uchaguzi tata, kulingana na ukaguzi wa jumuiya ya mataifa ya Amerika (OAS).

Wafuasi wa Evo Morales wakati wa maandamano katika mitaa ya Cochabamba, Novemba 18, 2019.
Wafuasi wa Evo Morales wakati wa maandamano katika mitaa ya Cochabamba, Novemba 18, 2019. RONALDO SCHEMIDT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Leo, Bolivia imegawanyika zaidi kuliko zamani kati ya wafuasi na wapinzani wa rais wa zamani Evo Morales.

Tangu ajiuzulu, rais wa zamani wa Bolivia anaishi uhamishoni na nchi hii imegawanywa kati ya wafuasi wake na wapinzani. Wafuasi wake wanadaia kiongozi wao (Evo Morales) arudi na kudai kwamba hatua ya Jeanine Añez, kujitangaza rais wa mpito wa Bolivia ni jaribio la mapinduzi. Wapinzani wa Morales wanataka hali ya utulivu irudi na kusisitiza kwamba serikali iliopo ni ya muda tu kabla ya uchaguzi mpya. Pande zote mbili zinaishi leo kwa uoga wa kulipiza kisasi.

Katika eneo la Satelito, moja ya maeneo ya El Alto, kwenye milima La Paz, sehemu kubwa ya wakaazi wake waliandamana dhidi ya Evo Morales. Wakati Evo Morales alipojiuzulu, makundi yanayomuunga mkono yalianazisha operesheni ya kulipiza kisasi dhidi ya wapinzani wa kiongozi huyo wa zamani.

Watu kadhaa ambao walishiriki maandamano dhidi ya Evo Morales tangu Novemba 10, walijikuta nyumba zao zimechomwa moto na mali zao kuharibiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.