Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-SIASA-HAKI

Nancy Pelosi: Trump atajiuzulu kama Nixon

Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani, Nancy Pelosi, amezungumza katika mahojiano yaliyorushwa Jumapili kuhusu kujiuzulu kwa Richard Nixon, akifananisha na hali ya sasa ya Donald Trump, ambaye pia anakabiliwa na shinikizo la kujiuzulu.

Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani, Nancy Pelosi, Oktoba 31, 2019.
Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani, Nancy Pelosi, Oktoba 31, 2019. REUTERS/Tom Brenner
Matangazo ya kibiashara

Nancy Pelosi ambaye ni kutoka chama cha Democratic, chenye viti vingi katika Baraza la Wawakilishi la Marekani aliwaambia waandishi wa habari wiki iliyopita kwamba la rais wa sasa wa Marekani kwa Ukraine kuhusu kuchunguza mpinzani wake katika uchaguzi wa rais wa Marekani mwaka ujao " ni sawa na kile alichokifanya Richard Nixon".

Katika mahojiano yaliyorushwa na kituo cha CBS Jana Jumapili, Nancy Pelosi ametaja matukio yanayofanana kati ya rais wa zamani kutoka chama cha Republican na rais wa sasa wa nchi hiyo Donald Trump.

"Nataka kusema, kile rais amefanya ni kibaya zaidi kuliko kile Richard Nixon alichofanya, kwa wakati fulani Richard Nixon alijutia vya kutosha nchi yake kwa kukubali kwamba hali hiyo haiwezi kuendelea," Nancy Pelosi amesema kwenye makala "Face the Nation".

Richard Nixon alijiuzulu mnamo mwaka 1974 kabla ya Baraza la wawakilisi kupiga kura kuhusu uwezekano wa kutimuliwa kwake. Mchakato huu dhidi yake ulifunguliwa kwa sababu ya kashfa ya Watergate kuhusu kuvamiwa kwa majengo ya Chama cha Democratic.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.