rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani Donald Trump

Imechapishwa • Imehaririwa

Kesi ya ung'atuzi dhidi ya Trump: Mahojiano ya wazi kuanza Novemba 13

media
Chumba ambacho kutafanyika mahojiano ya wazi ya kwanza ambayo yataanza wiki ijayo katika kesi ya ung'atuzi dhidi ya Donald Trump, Capitol, Washington. REUTERS/Joshua Roberts

Wabunge wa chama cha Democrats wametangaza kuanza kwa mahojiano ya wazi kuanzia wiki ijayo katika uchunguzi ambao unaweza kushuhudia rais Donald Trump akiondolewa madarakani.


Taarifa yao imeonesha kuwa maofisa watatu wajuu kutoka wizara ya mambo ya nje watatoa ushahidi, baada ya kuwa wamehojiwa kwa siri kwa majuma kadhaa.

Uchunguzi unaofanywa na wabunge umejikita katika madai kuwa rais Trump alimshinikiza rais wa Ukrain kutangaza hadharani kuanza uchunguzi dhidi ya mpinzani wake Joe Biden.

Mwenyekiti wa kamati ya Intelijensia, Adam Schiff ambaye anasimamia mchakato huu, amewaambia waandishi wa habari kuwa taratibu zote zimekamilika ambapo pia wamechapisha nyaraka za mahojiano waliyofanya na mashahidi watakaoitwa.

Rais Trump kwa upande wake amekosoa mchakato huu ulioanzishwa na Democrats akisema hakuna kosa alilofanya wakati wa maongezi yake na rais wa Ukraine, kauli anayoungwa mkono na baadfhi ya wabunge wa chama chake.