Pata taarifa kuu
BOLIVIA-MAANDAMANO-USALAMA

Bolivia: Maandamano yaongezeka, Umoja wa Mataifa watoa wito kwa utulivu

Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa raia wa Bolivia kudumisha amani wakati maandamano yanaendelea kushika kasi katika nchi hiyo ya Amerika ya Kusini.

Vizuizi vimewekwa kwenye moja ya mtaa wa mji wa La Paz, Bolivia Oktoba 29, 2019.
Vizuizi vimewekwa kwenye moja ya mtaa wa mji wa La Paz, Bolivia Oktoba 29, 2019. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Makabiliano mapya yaliibuka kati ya wafuasi na wapinzani wa Rais Evo Morales, aliyechaguliwa tena Oktoba 20 katika uchaguzi wenye utata.

Vizuizi, maandamano na mzozo: mzozo ambao umegawanya wananchi wa Bolivia kati ya wafuasi wa rais aliyepo madarakani tangu mwaka 2006 na upinzani ambao Jumanne wiki hii uliendelea kuingia mitaani kwa idadi kubwa ya waandamanaji, baada ya siku ya Jumatatu ambapo zaidi ya watu thelathini walijeruhiwa katika miji mitatu ya nchi hiyo, Santa Cruz, Cochabamba na La Paz.

Baada ya mji mkuu wa Bolivia, kukumbwa na maandamano makubwa Jumatatu wiki hii, hali hiyo ilishuhudiwa jana Jumanne katika mji wa Cochabamba, katikati mwa nchi, mji wenye wafausi wengi wa Rais Evo Morales. Makabiliano kati ya wafuasi na wapinzani waEvo Morales yamesababisha watu wengi kujeruhiwa, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Bolivia.

Umoja wa Mataifa umetoa wito, ukitaka pande husika "kusitisha uhasama na kudumisha amani mara moja", huku ukielezea "wasiwasi wake mkubwa baada ya kushuhudiwa machafuko makubwa katika maeneo mbali mbali ya nchi na (...) makabiliano kati ya raia".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.