Pata taarifa kuu
CHILE-USALAMA

Ghasia zaongezeka Chile, Piñera aonya maadui zake

Visa vya vurugu na uporaji vimeendelea jana Jumapili nchini Chile katika siku ya tatu ya ghasia mbaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo, na kusababisha vifo vya watu saba, ikwa ni pamoja na watu watano waliofariki katika kisa cha moto uliozuka katika kiwanda kimoja usiku wa kuamkia leo Jumatatu.

Kwa mara ya kwanza askari wa Chile wakipiga doria katika mitaa ya nchi hiyo tangu kumalizika kwa utawala wa kimla wa Jenerali Augusto Pinochet. Hapa ni katika mji wa Santiago Oktoba 20.
Kwa mara ya kwanza askari wa Chile wakipiga doria katika mitaa ya nchi hiyo tangu kumalizika kwa utawala wa kimla wa Jenerali Augusto Pinochet. Hapa ni katika mji wa Santiago Oktoba 20. REUTERS/Ivan Alvarado
Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji nchini Chile wamekasirishwa na kile wanachosema ni kupanda kwa gharama ya maisha, hali iliyochochewa baada ya serikali kupandisha nauli ya basi nchini humo.

Licha ya serikali kutangaza kuondoa nyongeza hiyo, waandamanaji wenye hasira wameendelea kupambana na maafisa wa usalama katika jiji kuu Santiago na miji mingine.

Kiwanda cha kutengeza ngu kimevamiwa na waandamanaji, ambao wamepora bidhaa na kukiteketeza kwa moto.

Wakati huo huo Rais wa Chile Sebastian Piñera amenyooshea kidolea cha lawama maadui zake akisema, mambo yameeleweka: nchi iko "vitani".

Kwa usiku wa pili mfululizo, serikali ya Chile imetamgaza hatua ya kutotoka nje usiku katika mji wa Santiago. kuanzaia saa moja usiku hadi saa kumi mbili asubuhi.

Wakati huo huo, "hali ya dharura" imetangazwa katika Majimbo matano, ikiwa ni pamoja na mji mkuu wenye wakaazi milioni 7. "Demokrasia ina jukumu la kujilinda," Rais wa Chile Sebastian Piñera amesema akitetea hatua hizi za dharura, baada ya mkutano na spika wa Baraza la wawakilishi, rais wa Bunge la Seneti na Seneti na rais wa Mahakama kuu.

Baadaye, rais Sebastian Piñera amezungumza mbele ya waandishi wa habari: "Tuko vitani na adui mwenye nguvu, ambaye haheshimu chochote wala mtu na ambaye yuko tayari kutumia vurugu na machafuko mengine bila kikomo. "

Jenerali Javier Iturriaga, ambaye alipewa majukumu ya kusimamia usalama wa umma na Rais Piñera Ijumaa wiki iliyopita, amewataka wakaazi kuwa "watulivu" na wasiondoke katika makaazi yao.

Machafuko mabaya ambayo hayajawahi kutokea nchini Chile kwa miongo kadhaa, yaliendelea Jumapili nchi humo. Makabiliano kati ya waandamanaji na maafisa wa polisi yalitokea katika eneo la Plaza Italia, katikati mwa mji wa Santiago, ambapo polisi walijibu kwa kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji

Wakati huo huo, visa vya uporaji vilishuhudiwa katika sehemu kadhaa za mji mkuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.