Pata taarifa kuu
MAREKANI-AJALI-USALAMA

Watu wengi wafariki dunia katika mkasa moto uliozuka katika meli California

Watu zaidi ya wanane wamefariki dunia jana Jumatatu asubuhi katika mkasa wa moto mkubwa uliozuka katika meli ya watalii kwenye pwani ya California. Watu wengine 26 hawajulikani waliko, vyanzo rasmi vimebaini.

Meli yenye urefu wa mita 22 iliyokuwa imeabiri watalii 39, ambayo imeteketea kwa moto katika bahari kwenye pwani ya California, Marekani.
Meli yenye urefu wa mita 22 iliyokuwa imeabiri watalii 39, ambayo imeteketea kwa moto katika bahari kwenye pwani ya California, Marekani. Service d'incendie du comté de Ventura / Document distribué via
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo mamlaka katika mji wa Barbara, katika Jimbo la California, ambako mkasa huo ulitokea, wanahofu kuwa idadi hiyo inaweza kuongezeka na kuwa kubwa zaidi kuliko ilivyotarajiwa. Meli hiyo ilikuwa ikisafiri karibu na kisiwa cha Santa Cruz, ambapo watalii walikuwa katika zoezi la kupiga mbizi. Tukio hilo lilitokea Jumatatu usiku.

Vyanzo kutoka idara ya huduma za dharura, vinabaini kwamba watu 39 walikuwa wakisafiri katikameli hiyo.

Miili minne ya watu waliofariki dunia imeopolewa kutoka majini, "ikiwa ni pamoja na wanaume wawili na wanawake wawili" ambao hawajatambuliwa rasmi, amesema Sheriff Brown.

"Waokoaji wameona miili minne chini ya bahari karibu na meli," ameongeza Sheriff Brown.

"Hivi sasa tuna timu za wapiga mbizi, ambao wanajaribu kuopoa miili hiyo, lakini bado kazi ni nzito na sina uhakika kuwa tutaweza kuopoa miili hiyo au miili mingine ambayo huenda imekwama katika meli, " amebaini Bill Brown.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.