Pata taarifa kuu
GUATEMALA-SIASA

Alejandro Giammattei ashinda uchaguzi wa urais Guatemala

Mgombea wa uchaguzi kutoka chama cha mrengo wa kulia cha Vamos nchini Guatemala, Alejandro Giammattei ameshinda uchaguzi wa urais uliofanyika jana Jumapili hii, Agosti 11. Uchaguzi huo ambao ulifanyika kwa duru ya pili ulishuhudia kiwango kidogo cha ushiriki.

Alejandro Giammatei katika makao yake makuu ya kampeni Guatemala City, Jumapili jioni Agosti 11.
Alejandro Giammatei katika makao yake makuu ya kampeni Guatemala City, Jumapili jioni Agosti 11. REUTERS/Jose Cabezas
Matangazo ya kibiashara

Alejandro Giammattei ameshinda kwa 58% ya kura, mbele ya Sandra Torres ambaye amepata 42% ya kura.

Ni mara ya nne mfululizo Bw Alejandro Giammattei kuwania kinyang'anyiro hicho cha urais. ameshinda uchaguzi huo baada ya kupambana vikali dhidi ya mshindane wake Asandra Torres, ambaye aliongoza katika duru ya kwanza ya uchaguzi, kwa mujibu wa mwandishi wetu katika kanda hiyo Patrick John Buffe.

"Lengo limefikiwa," alisema Alejandro Giammattei kutoka makao makuu ya kampeni Jumapili jioni, bila kusubiri kumalizika kwa zoezi la kuhesabu kura.

Baada ya kura 95 % kuhesabiwa, Alejandro Giammattei alipata 59% dhidi ya Sandra Torres, ambaye alikuwa akiwania nafasi hiyo kwa mara ya tatu. Bw Giammattei anatarajia kuchukuwa mikoba ya Jimmy Morales, ambaye muhula wake ulikumbwa na kashfa kubwa ya ufisadi. Anataraji kuchukuwa hatamu ya uongozi Januari 14, 2020.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.