Pata taarifa kuu
MAREKANI-SANAA

Toni Morrison, mkongwe wa fasihi afariki dunia

Toni Morrison, mwandishi wa kwanza Mmarekani mwenye asili ya Afrika aliyekabidhiwa Tuzo la Nobel kwa Fasihi, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88, familia yake imesema Jumanne wiki hii.

Mwandishi Mmarekani mwenye asili kutoka Afrika, Toni Morrison, aliyepata Tuzo ya Nobel kwa Fasihi.
Mwandishi Mmarekani mwenye asili kutoka Afrika, Toni Morrison, aliyepata Tuzo ya Nobel kwa Fasihi. Getty Images/Daniel Boczarski/FilmMagic
Matangazo ya kibiashara

"Toni Morrison amefariki dunia jana usiku, akizungukwa na familia yake na marafiki zake," imesema taarifa kutoka kwa familia yake.

Toni Morrison ambaye ni kutoka kizazi cha watumwa, anafahamika kwa kutoa mwonekano wa fasihi kwa watu weusi.

Msomi huyu mwenye kipaji cha hali ya juu ameandika riwaya 11 kwa kipindi cha miongo sita, lakini pia alijaribu kuandika, vitabu vya watoto, michezo miwili ya kuigiza na hata kitabu kidogo ambacho ni muhimu sana kwa maisha ya watu.

Aliweka wazi historia yote ya Wamarekani weusi tangu utumwa wao hadi kuingizwa katika jamii ya sasa ya Marekani.

Riwaya yake inayojulikana kama "Beloved" (Mpendwa), inaelezea historia ya mama ambaye alimwua binti yake ili kuepuka utumwa, ilipata tuzo ya Pulitzer mnamo 1988.

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama alimtunukia Toni Morrison tuzo ya medali ya kirais ya uhuru, moja ya tuzo kubwa yenye heshima zaidi nchini Marekani. Barack Obama amemtaja Toni Morrison kama "hazina ya kitaifa"

"Toni Morrison alikuwa hazina ya kitaifa, na mwandishi mzuri wa hadithi. Uandishi wake ulikuwa ni changamoto kubwa sana na dhamiri yetu na mawazo yetu ya maadili, "aliandika Barack Obama kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.