rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani Mauaji Donald Trump

Imechapishwa • Imehaririwa

Polisi yachunguza mashambulizi mawili ya watu kupigwa risasi Dayton na El Paso

media
Wakazi wa Dayton, Ohio, walikusanyika mnamo Agosti 4 baada ya mauaji yaliyokumba mji wao. REUTERS/Bryan Woolston

Maafisa nchini Marekani wanasema kuwa mashambulizi mawili ya watu kupigwa risasi yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita na kusabisha watu 29 kupoteza maisha na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa, yanachunguzwa iwapo kilikuwa ni kitendo cha ugaidi wa ndani.


Tayari mshukiwa mmoja amekamatwa akihusishwa na mauaji hayo katika mji wa El Paso katika jimbo la Texas.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema, mengi yanafanywa na serikali yake kudhibiti umiliki wa silaha, lakini amelaumu ongezeko la visa hivi kuchangiwa na matatizo ya akili miongoni mwa wanaomiliki silaha

“Tunaongea na watu wengi, na mambo mazuri yanafanyika na yapo njiani, tumefanya mengi lakini hayasemwi, lakini naamini mengi yanaweza kufanywa. Ukiangalia kwa kina, hili ni tatizo la kiakili na hawa ni watu ambao wanasumbuliwa sana na matatizo ya akili, ” Amesema Trump.

Shambulizi hilo linajiri katika muda wa saa 24, baada ya kutokea mkasa mwengine kama huo ambapo watu 20 waliuawa na 26 kujeruhiwa kwa kufyatuliwa risasi na mtu aliyekuwa na bunduki ndani ya duka moja kubwa eneo la El Paso, Texas.

Msemaji wa polisi wa El Paso Robert Gomez ameeleza kuwa wengi wa wahanga katika kisa cha Texas walimiminiwa risasi katika duka la Walmart.