Pata taarifa kuu
MAREKANI-BIASHARA HARAMU-HAKI

Madawa ya kulevya: El Chapo ahukumiwa kifungo cha maisha jela Marekani

Mahakama ya serikali kuu mjini Brooklyn nchini Marekani imemuhukumu kifungo cha maisha jela Joaquin "El Chapo" Guzman, mlanguzi sugu wa dawa za kulevya raia wa Mexico, baada ya kupatikana na hatia ya kufanya biashara ya kihalifu iliyosababisha vifo vya watu wengi na kuingiza nchini Marekani tani nyingi za madawa ya kulevya.

Mlanguzi sugu wa madawa ya kulevya "El Chapo", Mexico Januari 2016.
Mlanguzi sugu wa madawa ya kulevya "El Chapo", Mexico Januari 2016. REUTERS/Tomas Bravo/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Guzman mwenye umri wa miaka 62, pia ameamriwa kulipa dola milioni 12.6. Guzman alipatikana na hatia Februari mwaka huu kwa kusafirisha Marekani tani za cocaine, heroin na bangi na kuhusika katika njama za mauaji wakati akiwa kiongozi wa mtandao maarufu nchini Mexico wa biashara ya madawa za kulevya wa Sinaloa.

Jaji wa Marekani Brian Cogan ametangaza hukumu hiyo ya maisha pamoja na miaka 30.

Mahakama ya Shirikisho New York imemkuta El Chapo na hatia katika makosa 10, ikiwemo kusafirisha dawa za kulevya, utakatishaji fedha.

El Chapo alitoroko gerezani nchini Mexico mwaka 2016 na baadae kukamatwa na kuhamishiwa Marekani.

Mwezi Aprili 2017, baba mkwe wa Joaquin Guzman, alihukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani kwa kupenyeza bangi nchini Marekani.

Ines Coronel Barreras alipatikana na makosa katika mahakama moja ya Mexico, baada ya polisi kutwaa magari silaha na zaidi ya kilo 250 za bangi.

Marekani ilimwekea vikwazo miaka sita iliyopita, na kusema kwamba ni mojawepo wa vigogo wa genge la Sinaloa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.