Pata taarifa kuu
MAREKANI-UCHAGUZI-IASA

Elizabeth Warren aongoza mjadala wa kwanza wa kuwania kiti cha urais Marekani

Mbio za kuwania uteuzi wa kupeperusha bendera ya chama cha Democratic katika uchaguzi wa mwakani nchini Marekani zimeshika kasi, ambapo wagombea 10 kati ya ishirini wameshindana katika mdahalo wa televisheni.

Wanasiasa watano wa wa chama cha Democratic wachuana, Seneta Elizabeth Warren (katikati),  kwenye mjadala wa televiseni Juni 26, 2019.
Wanasiasa watano wa wa chama cha Democratic wachuana, Seneta Elizabeth Warren (katikati), kwenye mjadala wa televiseni Juni 26, 2019. REUTERS/Mike Segar
Matangazo ya kibiashara

Wagombea 10 kati ya 20 wamechuana usiku wa kuamkia leo katika mdahalo wa televisheni ambao ulitazamwa na mamilioni ya raia wa Marekai ambao watapima ikiwa wagombea hao wanastahili.

Wachambuzi wa masuala ya siasa nchini Marekani wanasema mwanamama Elizabeth Warren alifanikiwa pakubwa katika mdahalo wa hivi leo ambapo alijaribu kuzungumzia namna atakavyobadili sera za nchi hiyo kuhusu mambo ya nje na masuala ya wahamiaji.

Katika mdahalo huo wagombea karibu wote walijikita katika masuala ya msingi huku jina la rais wa Marekani Donald Trump likitajwa mara chache zaidi ukilinganisha na midahalo ya mwaka 2016.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.