rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani Iran Donald Trump Hassan Rouhani

Imechapishwa • Imehaririwa

Ripoti: Rais Trump alikuwa ameagiza ndege za kivita kuishambulia Iran

media
Rais wa Marekani Donald Trump REUTERS/Leah Millis

Vyombo vya Habari nchini Marekani vinaripoti kuwa, rais wa Marekani Donald Trump alikuwa ameidhinisha mashambulizi ya kijeshi dhidi ya  Iran, lakini baadaye akabadilisha mawazo yake.


Gazeti la New York limemnukuu afisa wa juu kutoka Ikulu ya Marekani akisema kuwa mashambulizi hayo, yalikuwa yafanyike katika maeneo kadhaa nchini Iran kabla ya Trump kubadilisha uamuzi huo.

Hata hivyo, Ikulu ya Marekani haijazungumzia ripoti hiyo.

Hatua hii inakuja, baada ya Iran kuiangusha ndege ya Iran isiyokuwa na rubani, iliyokuwa inapaa katika angaa lake.

Tehran imekiri kuiangusha ndege hiyo isiyokuwa na rubani, baada ya kuonekana ikipaa katika angaa lake, lakini Marekani inasema ndege hiyo ilikuwa katika angaa la Kimataifa lisilokuwa na mwenyewe.

Wasiwasi umeendelea kushuhudiwa kati ya Marekani na Iran, baada ya Washington DC kudai kuwa Tehran ilishambulia meli za mafuta katika Ghuba ya Oman.

Wakati uo huo, Iran imetishia kuendelea na mpango wake wa kurutubisha Uranium, kinyume na mkataba wa Kimataifa wa mwaka 2015, uliozuia urutubishaji huo kwa angalau miaka 10 kwa sababu za kiusalama.