rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani Iran Mike Pence Hassan Rouhani

Imechapishwa • Imehaririwa

Marekani yasema haina mpango wa kuingia kwenye vita na Iran

media
Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo akisalimiana na mwenzake Sergueï Lavrov, walipokutana mjini Sochi tarehe 14 mwezi Mei 2019 Pavel Golovkin/Pool via REUTERS

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amesema nchi yake haina mpango wa kuingia kwenye vita na Iran, licha ya wasiwasi unaoshuhudiwa kati ya nchi hizo mbili.


Akizungumza akiwa nchini Urusi, Pompeo amesema shinikizo na vikwazo dhidi ya Iran ni kuifanya nchi hiyo kuwa kama nchi ya kawaida.

“Hatuna mpango wa kuingia kwenye vita dhidi ya Iran, kinachofanyika ni kuhakikisha kuwa nchi hiyo inakuwa kama nchi ya kawaida,” alisema Pompeo.

Wakati uo huo, kiongozi wa kiroho wa Iran Ayatollah Ali Khamenei naye amesema kuwa nchi hiyo haifanyi maandalizi yoyote ya kupigana na Marekani.

Kumekuwa na wasiwasi wa kutokea kwa vita kati ya nchi hizo mbili baada ya Marekani wiki iliyotuma kutuma zana zake za kivita kama manuari na ndege katika pwani ya mataifa ya ghuba.

Marekani ilijiondoa kwenye mkataba wa Kimataifa wa mwaka 2015 ulioruhusu Iran kutoendelea na mradi wake wa kurutubisha uranium, mkataba ambao uongozi wa rais Donald Trump hauridhishi na ni hatari kwa usalama wa dunia.

Iran imekiri kuwa vikwazo kutoka Marekani, vimeathiri uchumi wake.