Pata taarifa kuu
VENEZUELA-MAREKANI-MADURO-SIASA-USALAMA

Marekani yaendelea na shinikizo dhidi ya Maduro

Makamu wa rais wa Marekani, Mike Pence, anatarajia kutangaza leo Jumanne hatua mpya ya kuhamasisha jeshi la Venezuela kutoendelea kumuunga mkono rais wa Venezuela Nicolas Maduro, mwakilishi mwandamizi wa utawala wa Marekani ameliambia shirika la habari la Reuters.

Makamu wa rais wa marekani Mike Pence aendelea kumuonya rais wa Venezuela Nicolas Maduro.
Makamu wa rais wa marekani Mike Pence aendelea kumuonya rais wa Venezuela Nicolas Maduro. REUTERS/Ammar Awad
Matangazo ya kibiashara

Wakati jaribio la kukaidi serikali lililopangwa na kiongozi wa upinzani Juan Guaido, ambaye alijitangaza rais wa mpito wa nchi hiyo lilishindwa wiki iliyopita, Mike Pence pia anatarajia kuonya utawala wa Maduro kwamba Marekani inajiandaa kuweka vikwazo dhidi ya majaji 25 wa Mahakama Kuu, ameongeza mwakilishi huyo, ambaye hakutaja jina lake.

Wakati wa hotuba yake Jumanne hii mchana, Makamu wa rais wa Marekani pia atatoa msaada kwa wakimbizi wa Venezuela ambao wameitoroka nchi hiyo ya Amerika ya Kusini.

Juan Guaido anaendelea kukumbwa na upinzani kutoka vikosi vya jeshi na polisi tangu alipotambuliwa mnamo mwezi Januari kama rais halali wa Venezuela na nchi nyingi za Magharibi, zikiongozwa na Marekani, na nchi jirani za Venezuela, kama vile Brazil na Colombia.

Kiongozi wa upinzani nchini Venezuela alisema Jumatano kuwa Nicolas Maduro hana tena uungwaji mkono wa jeshi. Hata hivyo, hakuna dalili zinazoonyesha kuwa maafisa wa ngazi ya juu katika jeshi wamebadili msimamo.

Mbali na jeshi, Nicolas Maduro ana uungwaji mkono kutoka Urusi, China, Cuba na Uturuki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.