Pata taarifa kuu
VENEZUELA-SIASA-UCHUMI

Venezuela: Juan Guaido aondolewa kwenye nafasi yake ya Spika wa Bunge

Spika wa Bunge la Venezuela Juan Guaido, pia kiongozi wa upinzani, ameondolewa kwenye nafasi yake na hatoweza kushikilia nafasi yoyote anayepewa mtu aliyechaguliwa, kwa muda wa miaka 15 kwa madai ya rushwa, mamlaka nchini Venezuela imesema.

Juan Guaido katika kikao cha Bunge la Venezuela Machi 6, 2019 Caracas.
Juan Guaido katika kikao cha Bunge la Venezuela Machi 6, 2019 Caracas. REUTERS/Ivan Alvarado
Matangazo ya kibiashara

Mkaguzi Mkuu wa serikali Elvis Amoroso, anayehusika na masuala ya uwazi katika utawala nchini Venezuela, ameamua "kuzuia nafasi zote anazoweza kusimamia mtu aliyechaguliwa kwa mwananchi (Juan Guaido) kwa kipindi cha juu kilichotolewa na sheria" Amoroso ametangaza kwenye televisheni ya serikalii katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Alhamisi jijini Caracas.

Kwa mujibu wa Elvis Amoroso, Juan Guaido hajatoa maelezo kuhusu gharama za safari zake za nje ya nchi na fedha anazopata kutoka nchi nyingine. "Alifanya safari zaidi ya 91 nje ya nchi kwa gharama kubwa kuliko bolivar milioni 570 (sawa na dola za Marekani 168,000 kwa bei ya sasa) bila kutoa maelezo wapi fedha hizo zimetoka," amesema Mkaguzi Mkuu wa serikali, akiongeza kuwa Juan Guaido "alitumia mamlaka aliyopewa na wananchi na kufanya vitendo na serikali za kigeni ambazo zimewatia hatarini wananchi wa Venezuela.

Juan Guaidó amefutilia mbali adhabu hiyo, "yeye si mkaguzi wa serikali" amesema, "Bunge pekee ndio halali ya kuteua Mkaguzi Mkuu wa serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.