rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Venezuela Nicolas Maduro Juan Guaido

Imechapishwa • Imehaririwa

Venezuela yaendelea kukumbwa na kiza kinene

media
Miji kadhaa ya Venezuela yaendelea kusalia bila umeme. REUTERS/Carlos Jasso

Umeme umeendelea kukatwa katika maeneo mengi nchini Venezuela, hali inayosababisha mtafaruku nchini humo, huku upinzani na utawala wakiendelea kushtumiana kuhusika na hali hiyo.


Kulingana na vyombo vya habari nchini Venezuela,umeme umekatika katika majimbo 22 kati ya majimbo 23 na hivyo kuiacha karibu nchi nzima bila umeme.

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa hali kama hiyo haijatokea nchini Venezuela kwa miaka mingi.

Kukatika kwa umeme kumesababishwa na matatizo katika bwawa la Guri kusini mwa jimbo la Bolivar, kwa mujibu wa chanzo cha mamlaka ya umeme ambacho hakikutaja jina.

Bwawa la Guri ni kati ya mabwawa muhimu ya kusambaza umeme nchini Venezuela, chanzo hicho kimeongeza.

Hata hivyo waziri wa umeme Luis Motta Dominguez amesema kuwa hilo sio shambulizi dhidi ya serikali bali ni shambulizi dhidi ya wananchi, huku akinyooshea kidole cha lawama upinzani.

Hali hiyo inatokea siku tano baada ya kiongozi wa upinzani Juan Guaido kujaribu kukutana na vyama vikuu vya wafanyakazi.