rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani Donald Trump

Imechapishwa • Imehaririwa

Mkurugenzi wa zamani wa kampeni ya Trump ahukumiwa miezi 47 jela

media
Mkurugenzi wa zamani wa kampeni wa Donald Trump, Paul Manafort, Washington, tarehe 15/06/2018. REUTERS/Jonathan Ernst

Aliyekuwa Meneja wa kampeni za rais wa Marekani Donald Trump mwaka 2016, Paul Manafort amehukumiwa jela miezi 47 katika kesi yake ya kwanza.


Mahakama imemhukumu kifungo hicho, baada ya kumpata na kosa la kukwepa kodi lakini pia kufanya udanganyifu katika masuala ya benki.

Hukumu hiii imetolewa baada ya kupatikana na kosa la kuficha Mamilioni ya Dola, baada ya kulipwa na kutoa ushahidi wa kisiasa nchini Ukraine.

Ni hatua inachukuliwa na Mahakama, wakati huu Tume maalum ikiendelea kuchunguza iwapo Manafort alishiriki kwa vyovyote vile na madai kuwa, Urusi ilimsaidia rais Trump kushinda Uchaguzi wa mwaka 2016.

Mbali na kifungo hicho, anatarjiwa kulipa faini ya dola 50,000.

Hata hivyo, akizungumza Mahakamani baada ya hukumu hiyo Manafort amesema amekuwa na kipindi kigumu kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita, na alitaka Jaji kumwonea huruma.

Viongozi wa Mashtaka walikuwa wanataka afungwe jela kati ya miaka 19 hadi 24 lakini Jaji akasema, hilo halingewezekana.