Pata taarifa kuu
VENEZUELA-SIASA-UCHUMI

Mike Pompeo: Siku za Maduro kukaa madarakani zinahesabika

Shinikizo la kimataifa limeongezeka dhidi ya kiongozi wa Venezuela Nicolas Maduro, huku serikali ya Washington ikisisitiza kuwa siku za kiongozi huyo zinahesabika baada ya jitihada za upinzani kuingiza misaada ya kibinadamu nchini humo kugubikwa na umwagaji damu.

Kiongozi wa upinzani Juan Guaido, aliyejitangaza rais wa mpito wa Venezuela, akiwasili katika kambi ya kijeshi ya Colombia huko Catam, karibu na Bogotá, akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Colombia Carlos Holmes Trujillo, Februari 24, 2019.
Kiongozi wa upinzani Juan Guaido, aliyejitangaza rais wa mpito wa Venezuela, akiwasili katika kambi ya kijeshi ya Colombia huko Catam, karibu na Bogotá, akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Colombia Carlos Holmes Trujillo, Februari 24, 2019. Courtesy of Colombian Presidency/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa upinzani aliyejitangaza kuwa Rais wa mpito Juan Guaido ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua stahiki kwa le kinachoendelea nchini Venezuela baada ya makabiliano ya kuvuka mpakani kusababisha vifo vya watu wanne.

Umoja wa Ulaya umelaani matumizi ya nguvu na vikosi vyenye silaha kuzuia misaada kufikia wahitaji nchini Venezuela.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amesema ameshtushwa na kuhuzunishwa na vifo vya raia wanne.

Hayo yanajiri wakati huu Guaido akitaraji kuhudhuria mkutano wa Bogota utakaowaweka pamoja viongozi wa nchi za Amerika Kusini, huku akitoa wito kwa jamii ya kimataifa kujiandaa kwa lolote litakalowezekana dhidi ya Maduro.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.