Pata taarifa kuu
MAREKANI-MEXICO-SIASA

Hali ya dharura: California yafungua mashitaka dhidi ya utawala wa Trump

Utawala wa Donald Trump unaendelea kubanwa kuhusu ujenzi wa ukuta kwenye mpaka na nchi jirani ya Mexico, baada ya rais Trump kutangaza hali ya dharura kwenye mpaka huo.

Donald Trump akiwa El Paso, Texas, mbele ya mashabiki wake. Februari 11, 2019.
Donald Trump akiwa El Paso, Texas, mbele ya mashabiki wake. Februari 11, 2019. REUTERS/Leah Millis
Matangazo ya kibiashara

Hali ya dharura inamuwezesha rais wa Marekani Donald Trump, ambaye lengo lake kubwa ni kujenga ukuta kwenye mpaka kati ya Marekani na Mexico, kupata fedha kutoka serikali ya shirikisho. Lakini Majimbo kadhaa tayari yametangaza nia yao ya kufungua kesi dhidi ya utawala wa Trump ili kuzuia mpango huo.

Vita dhidi ya hali ya dharura iliyotangazwa na rais Donald Trump inatarajia kuibuka katika bunge la wawakilishi na mbele ya mahakama mbalimbali nchini Marekani. Tangazo hilo "ni aibu kwa taifa," Gavana wa California ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Pamoja na Majimbo mengine kadhaa, ikiwa ni pamoja na New York, Gavana wa California, Gavin Newsom ameahidi kufungua mashtaka dhidi ya serikali, mapema wiki hii.

Kwa mujibu wa Gavin Newsom, hakuna hali ya dharura au mgogoro wa wahamiaji kwenye mpaka wa Mexico. Idadi ya wahamiaji haramu wanaovuka mpaka na kuingia nchini Marekani imepungua kwa kiasi kikubwa tangu miaka thelathini iliyopita, hivyo mgogoro unaotajwa umetengenezwa na rais Donald Trump mwenyewe katika kutekekeza ahadi yake ya kampeni, amesema Gavin Newsom.

Baada ya siku 35 za kukwama kwa shughuli za serikali nchini Marekani na kushindwa kwa vita vya kwanza vya kisiasa, mpango huu wa hali ya dharura unamuwezesha Donald Trump kutopingwa na bunge la Congress ili kupata dola Bilioni 7 katika bajeti ya Pentagon lakini pia katika fedha za misaada kwa majanga ya asili na kupambana na madawa ya kulevya, ili kujenga ukuta wake dhidi ya wahamiaji.

Wabunge kutoka chama cha Democratic ambao ndio wengi bungeni wameahidi kuwa watazuia mpango huo wa Donadl Trump.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.