Pata taarifa kuu
VENEZUELA- EU-MAANDAMANO-SIASA

Nchi kadhaa za Ulaya zamtambua Juan Guaido kama rais wa Venezuela

Baada ya Waziri Mkuu wa Uhispania, rais wa Ufaransa amemtambua Juan Guaido kama rais halali wa Venezuela. Bunge la Uingereza tayari limetangaza kwamba linamtambua Juan Guaido kama rais wa Venezuela.

Maandamano ya kumuunga mkono Juan Guaido, Caracas, Februari 2, 201
Maandamano ya kumuunga mkono Juan Guaido, Caracas, Februari 2, 201 REUTERS/Luisa Gonzalez
Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati muda wa mwicho uliyowekwa na nchi kadhaa za Ulaya ulimalizika Jumapili usiku Februari 4. Nchi hizo zilimtaka rais Nicolas Maduro kuitisha uchaguzi mpya wa haraka la sivyo zitamtambua Juan Guaido kama rais halali wa Venezuela.

Wakati huo huo Urusi imekosoa msimamo huo wa nchi za Ulaya na kushtumu kwamba zimeingiliamasuala ya ndani ya Venezuela.

Tangu Jumatatu hii Februari 4 nchi kadhaa za Ulaya, ikiwa ni pamoja na Ufaransa, Uhispania, Uingereza na Ujerumani zimemtambua Juan Guaido kama rais halali wa Venezuela.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.