Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI-UCHUNGUZI

Uchunguzi wa Urusi: Mshauri wa zamani wa Trump kuepuka jela

Mwendesha mashtaka maalum anayehusika na uchunguzi wa Urusi Robert Mueller amependekeza hukumu bila kifungo dhidi ya Michael Flynn, aliye kuwa mshauri katika masuala ya usalama wa taifa wa Donald Trump, kutokana na "msaada wake mkubwa" katika uchunguzi.

LAliye kuwa Mshauri wa usalama wa taifa wa rais Donald Trump, Jenerali Michael Flynn.
LAliye kuwa Mshauri wa usalama wa taifa wa rais Donald Trump, Jenerali Michael Flynn. REUTERS/Yuri Gripas/File Photo
Matangazo ya kibiashara

"Kutokana na msaada mkubwa wa mtuhumiwa (...), ninapendekeza hukumu dhidi yake bila kifungo" amesema mwendesha mashitaka kwenye waraka ambao aliwasilisha mahakamani.

Michael Flynn, mshauri wa zamani wa Trump wakati wa uchaguzi na mshauri wa zamani wa usalama wa taifa wa rais wa Donald Trump kwa muda wa siku 22, alikiri mwaka 2017kuwa alidanganya shirika la ujasusi la FBI, ikiwa ni pamoja na mazungumzo yake na balozi wa Urusi nchini Marekani Sergei Kislyak. Alikubaliana pia kushirikiana na mahakama.

"Mtuhumiwa alisaidia katika uchunguzi unaoendelea," hati ya mahakama inaeleza, ikitaja uchunguzi wake "kuhusu uhusiano kati ya serikali ya Urusi na watu binafsi walioteuliwa katika timu ya kampeni ya Rais Donald J. Trump."

Rais Trump amekuwa akisema, uchunguzi huo umechochewa kisiasa, na kusisitiza kuwa Urusi haikuwahi kumsaidia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.